Bondia Iddy Mkwera akinyooshwa mkono juu baada ya kumgaragaza Lucas Ndula, wakati wa mpambano wa mabondia wa Dar na Muheza. Mkwera alishinda kwa pointi mpambano hou wa raundi sita, uliotayarishwa kwa ajili ya kuinua mchezo wa ngumi, wilayani Muheza na pia kusherekea Sikukuu ya Pasaka.
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Iddy Mkwera wa Dar es Salaam, ameibuka mshindi baada ya kumgaragaza bondia Lucass Ndula wa Muheza wakati wa mpambano wa kuhamasisha masumbwi, wilayani Muheza uliochezwa wakati wa Siku kuu ya Pasaka katika Uwanja wa Jitegemee, mkoani Tanga.
Mpambano ulioanza kwa Ndula kuanza kwa kasi na kushangiliwa na wapenzi wengi katika raundi ya kwanza na ya pili upepo ulianza kumbadilikia, raundi ya tatu baada ya kukata pumzi huku akitupa ngumi bila mpangilio, wakati Mkwera akipanga mashambulizi na kupiga ngumi kali na za kushitukiza zilizo mfanya Ndula kutulia.
Raundi ya tano, ilikuwa ni mfululizo wa makonde yaliyorushwa na Mkwera katika kumuadhibu Ndula na ilipofika raundi ya sita na ya mwisho wa mchenzo huo, Ndula alipigwa upercut, ambayo ilimchanganya na kufanya kuwa nje ya mchezo kwa kushika magoti.
Bondia huyo aliokolewa na kengele iliyoashiria kumaliza mpambano huo wa raundi sita na kufanya Iddy Mkwera kuibuka na ushindi wa point akipeperusha vema bendera ya Dar es Salaam katika wilaya ya Muheza, mkoani Tanga.
Mfadhili wa mpambano huo, ambaye aliwezesha kufanikisha kila kitu kinachohitaji katika mpambano huo, ikiwemo kupeleka mabondia kutoka Dar pamoja na ulingo uliotumika, maalumu kwa ajili ya masumbwi, Allan Augostino ameahidi kurudia kufanya onesho hilo, la wazi katika Viwanja hivyo hivyo vya Jitegemee, Muheza mkoani Tanga, wakati wa Siku kuu ya Iddi na kuwataka wapenzi kujitokeza kwa wingi katika mpambano huo ujao.
Mpambano huo, uliofanyika katika Viwanja vya wazi vya Jitegemee, uliwavuta wapenzi wengi, wakiwemo watoto, vijana na wazee na kujitokeza kwa wingi kuangalia mchezo huo.
|
No comments:
Post a Comment