Pages

Wednesday, April 17, 2013

Bi. Kidude afariki dunia kisiwani Zanzibar



Bi. Fatma Bint Baraka 'Bikidude', wakati wa uhai wake 


Nguli wa Muziki wa Mwambao nchini, barani Afrika pamoja na Ulaya katika fani ya Muziki wa Taraab Fatuma Binti Baraka maarufu kwa jina la Bi Kidude ambaye amefariki akiwa na miaka zaidi ya 98. amefariki mchana huu.huko maeneo ya Bububu Kihinani kwa jamaa zake katika nyumba ya Mjukuu wake Baraka.

Kwa taarifa tulizozipata kupitia kwa jamaa wa marehemu wamesema Bi Kidude katika wiki hii alikuwa amezidiwa na kumpeleka katika Hospitalya Kibweni ya KMKM, kwa matibabu. na kuruhusiwa kurudi nyumba.

Jamaa wa marehemu wamesema Bikidude amefariki leo majira ya saa saba mchana huko kihinani na memehamishiwa nyumbani kwake kwa ajili ya mazishi kesho mchana katika majira ya saa 7.00 na kuzikwa katika makaburi ya Kitumba Mkoa wa Kusini Unguja Wilaya ya Kati.

Mipango ya mazishi inafanyika Nyumbani kwake Rahaleo..

Bi Kidude aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa uvimbe na kisukarin kwa mujibu wa jamaa wa marehemu walivyosema. kulazwa mara kadhaa kifo chake kinaelezwa pia kuchangiwa zaidi na umri mkubwa.

Msiba huu ni mzto kuwahi kutokea kwa tasnia ya muziki na Sanaa kwa ujumla kufuatia Mchango mkubwa wa Marehemu katika kukuza muziki halisia wa mwambao.

Rais Jakaya Kikwete alimtunuku Bi Kidude Nishani ya Uhuru wa Tanzania kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika kipindi cha uhai wake.

No comments:

Post a Comment