Na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo Machi 31, 2013 ametembelea Hospital ya Taifa ya Muhimbili kuwapa pole majeruhi walioumia katika ghorofa lililoporomoka juzi Ijumaa Machi 26, 2013 katika Mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 20.
Rais Kikwete, akiwa ameongozana na mke wake, Mama Salma Kikwete, pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Mhe. Hawa Ghasia, aliwatembelea na kuwapa pole majeruhi Mohamed Ally Dhamji, Baqir Virani, Selemani Saidi na Yusuf Abdallah waliolazwa Taasisi ya Mifupa (MOI).
Majeruhi hao, ambao kwa mujibu wa Daktari C.N. Mcharo wanaendelea vyema na matibabu na hali zao ni za kuridhisha, ni wanne ni kati ya sita waliolazwa katika taasisi hiyo, ambapo wawili wamekwisharuhusiwa.
"Poleni sana kwa maumivu mliyoyapata na nawatakia mpate nafuu ya haraka", Rais Kikwete aliwaeleza majeruhi hao, walionusurika baada ya kuangukiwa na jengo hilo la ghorofa 16 lililoporomoka ghafla likiwa katika ujenzi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe, Mama Salma Kikwete wakiwasili katika wodi ya Taasisi ya Mifupa ya MOI, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Salaam leo, kuwajulia hali vijana Mohamed Ally Dhamji (kushoto), Baqir Virani, ambao ni kati ya majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji, Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe, Mama Salma, wakiwa katika wodi ya Sewa Haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es salaam leo, Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole Selemani Saidi, mmoja wa majeruhi walionusurika katika ajali ya jengo lililoporomoka katikati ya jiji, Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25. Kushoto mwenye suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa Taasisi ya Mifupa ya Moi.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akimpa pole Selemani Saidi, mmoja wa majeruhi walionusurika katika ajali ya jengo lililoporomoka katikati ya jiji, Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25, wakati Rais na Mama Salma walipotembelea katika wodi ya Sewa Haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, kuwajulia hali majeruhi hao leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe, Mama Salma, wakiwa katika wodi ya Taasisi ya Mifupa ya MOI, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam leo, wakimpa pole kijana Mohamed Ally Dhamji, ambaye ni miongoni mwa majeruhi walionusurika katika ajali ya jengo lililoporomoka katikati ya jiji, Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakimjulia hali kijana Mohamed Ally Dhamji, ambaye ni miongoni mwa majeruhi walionusurika katika ajali ya jengo lililoporomoka katikati ya jiji na kusababisha vifo vya watu 25.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe, Mama Salma Kikwete wakizungumza na kijana Mohamed Ally Dhamji, ambaye ni miongoni mwa majeruhi walionusurika katika ajali ya jengo lililoporomoka katikati ya jiji na kusababisha vifo vya watu 25.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe, Mama Salma Kikwete wakizungumza na kijana Mohamed Ally Dhamji, ambaye alikuwa miongoni mwa majeruhi walionusurika katika ajali ya jengo lililoporomoka katikati ya jiji na kusababisha vifo vya watu 25, wakati Rais alipowatembelea majeruhi hao, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe, Mama Salma, wakimpa pole Yusuf Abdallah ambaye ni mmoja wa majeruhi walionusurika katika ajali ya jengo lililoporomoka katikati ya jiji, Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25, wakati alipofika wodi ya Sewa Haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Hawa Ghasia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma, wakiwa katika wodi ya Sewa Haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam leo, Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole kijana Baqir Dhamji, mmoja wa majeruhi walionusurika katika ajali ya jengo lililoporomoka jijini Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita. Kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa Taasisi ya Mifupa ya MOI.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe, Mama Salma wakimuaga kijana Mohamed Ally Dhamji ambaye ni miongoni mwa majeruhi walionusurika katika ajali ya jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25.
No comments:
Post a Comment