Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amelazwa tena
hospitalini baada ya kuugua ugonjwa wa mapafu kwa mara nyingine.
Taarifa kutoka kwa serikali ya nchi hiyo, ilisema kuwa Mandela mwenye umri wa
miaka 94 alilazwa hospitalini muda mfupi kabla ya saa sita usiku.Anasifika sana kama baba wa taifa hilo kwa kuongoza vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Kadhalika Mandela alihudumu kama rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini tangu mwaka 1994 hadi mwaka 1999, ingawa hali yake ya kiafya imezua wasiwasi kwa muda sasa.
Rais Jacob Zuma alimtumia taarifa ya kumpa pole na kumtakia kupona Mandela
"tunawataka watu wa Afrika Kusini pamoja na duniani kote kuwa watulivu na kumuombea Madiba na familia yake.
Tuna imani kuwa kikosi cha madaktari wanaomtibu Mandela watafanya kila hali kuhakikisha anapona,'' alisema Zuma katika taarifa yake.
Mapema mwezi huu bwana Mandela alilazwa hospitalini mjini Pretoria baada ya kufanyiwa ukaguzi wa kiafya.
No comments:
Post a Comment