Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Gaston
Makuzangba, ameiambia BBC kwamba mji mkuu, Bangui, umejitayarisha kwa shambulio
lolote la wapiganaji.
Msemaji huyo alieleza kuwa kila njia inatumika kuuhami mji mkuu lakini wanajeshi wamewazuwia wapiganaji wa kundi la Seleka kilomita 70 kaskazini-mashariki ya Bangui.
Hata hivyo kamanda wa wapiganaji, Arda Akouman, alisema Seleka wako kama kilomita 18 tu nje ya Bangui na wanataraji kufika mji mkuu usiku wa Jumamosi.
Aliwaomba watu wawe watulivu na jeshi liweke silaha chini.
Kuna taarifa piya za mapigano huko Boussambele, kilomita 160 kaskazini-magharibi ya Bangui.
No comments:
Post a Comment