Naibu Waziri wa Habari,
Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala akimkabidhi kombe la Ubingwa wa
michuano ya NSSF Media Cup 2013, Naodha wa timu ya Jambo Leo, Said Mwishehe
baada ya kuifunga Changamoto bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika
leo, kwenye Viwanja vya Sigara (TCC), Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari,
Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa
michuano ya NSSF Media Cup 2013, Naodha wa timu ya Business Times Queens,
Lulu Habibu baada ya timu hiyo, kuifunga TBC vikapu 39-18 katika mchezo wa fainali kwa uapnde wa Netibali, uliofanyika leo
kwenye Viwanja vya Sigara (TCC), Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo,
Amosi Makala akikagua timu ya Business Times Queens kabla ya mchezo wao dhidi ya
TBC.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo,
Amosi Makala akikagua kikosi cha timu ya TBC Queens.
Kikosi cha TBC Queens kikiwa
katika picha ya pamoja.
Mabingwa wa Netiboli wa Kombe
la NSSF Media Cup 2013 Business Times Queens kikiwa katika picha ya pamoja kabla
ya kuumana na TBC katika fainali.
Mabingwa wa soka wa michuano
ya NSSF Media Cup 2013, Jambo Leo, katika picha ya pamoja kabla ya mechi ya
fainali dhidi ya Changamoto.
Kikosi cha timu ya Changamoto
kilichoshika nafasi ya pili NSSF Media Cup 2013
Beki wa Changamoto John
Robert akichuana na mshambuliaji wa Jambo Leo, Rogatius Katyali katika mchezo wa
fainali ya michuano ya NSSF Media Cup 2013.
Wachezaji wa timu za TBC na
(jezi nyeupe) na BTL wakichuanba katika mchezo wa fainali ya netiboli ya
michuano ya NSSF Media Cup 2013.
Wachezaji wa Jambo Leo
wakifurahia Kombe la ushindi baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala, viwanjani hapo.
Mashabiki wa timu ya Netiboli
ya Business Times wakishangilia ushindi wa timu yao.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhani Dau akizungumza wakati wa hafla ya
kufunga michuano ya NSSF Media Cup 2013 leo.
Naibu Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Amosi Makala akizungumza katika hafla ya kufunga
michuano ya NSSF Media Cup 2013 leo. (Picha zote na Habari Mseto Blog)
DAR ES SALAAM,
Tanzania
TIMU za Jambo Leo na Business
Times (BTL), leo zimefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya NSSF Media Cup 2013,
baada ya kushinda mechi zao za fainali ya soka na netiboli dhidi ya Changamoto
na TBC.
Katika fainali ya soka, bao
pekee la kipindi cha kwanza la mshambuliaji Julius Kihampa, lilitosha kuwapa
Jambo Leo ubingwa wa pili wa michuano hiyo iliyofanyika kwa mwaka wa 10 na
harakati za Changamoto kusawazisha hazikuzaa matunda.
Kwa upande wa Netiboli,
Business Times Queens ‘The Bize,’ ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mchezo huo kwa
ushindi wa magoli 39-18 dhidi ya TBC, huku nyota wake Lulu Habibu akifunga mara
27.
Lulu alitwaa tuzo ya mfungaji
bora wa michuano hiyo upande wa netiboli kwa kufikisha magoli 153 katika mechi
nne alizocheza, huku tuzo hiyo kwa upande wa soka ikitwaliwa na Nurdin Msindo wa
Tumaini Media, aliyefunga mabao manne.
Lulu na Nurdin kila mmoja
alizawadiwa kiasi cha shilingi 300,000 ambayo ni zawadi kwa wafungaji bora, huku
Sahara Media ikitwaa tuzo ya timu yenye nidhamu, ambapo walizawadiwa
kikombe.
Kwa kutwaa ubingwa soka,
Jambo Leo walizawadiwa kikombe na shilingi mil. 4, huku Changamoto wakitwaa
shilingi mil. 3 kwa kushika nafasi ya pili na TBC wakizoa shilingi mil. 2 kwa
kutwaa nafasi ya tatu - baada ya juzi Ijumaa kuwalaza IPP kwa penati
4-3.
‘The Bize Queens’, wamebeba
kombe na shilingi mil. 3.5 za ubingwa wa netiboli, huku mshindi wa pili TBC
wakilamba shilingi mil. 2 na mshindi wa tatu NSSF wakibeba kombe pekee na kitita
chao cha shilingi mil. 1 wakikitoa kwa Tumaini iliyoshika nafasi ya
nne.
NSSF Media Cup 2013 ni
michuano iliyofanyika kwa wiki mbili kwenye viwanja vya TCC na DUCE vilivyoko
Chang’ombe jijini Dar es Salaam, ikihusisha timu 17 za soka na 15 za netiboli
zilizoundwa na wafanyakazi wa vyombo vya habari nchini.
Baada ya michuano hiyo
kuzinduliwa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaundencia Kabaka Machi 9, ilihitimishwa
leo kwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makalla
kukabidhi zawadi kwa washindi wapya.
No comments:
Post a Comment