TANGAZO


Thursday, March 21, 2013

Jambo Leo yaidhibu TBC, Nusu Fainali Michuano ya NSSF

Golikipa wa timu ya Jambo Leo, Semeni Selemani, akiondoa hatari iliyoelekezwa langoni kwake na wachezaji wa timu ya TBC, katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Kombe la NSSF, Uwanja wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu (DUCE), Chang'ombe, Dar es Salaam jana. Jambo iliiadhibu TBC mabao 2-0. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Mwalimu wa timu ya Jambo Leo, Jerry Kotto, akiwapa maelekezo wachezaji wa timu hiyo, wakati wa mapumziko, wakati huo Jambo ilikuwa mbele kwa bao 1-0. 

 Mwalimu wa timu ya Jambo Leo, Jerry Kotto, akitoa maelekezo kwa wachezaji wa Jambo Leo.
Mwalimu Jerry akisisitiza jambo, wakati akitoa maelekezo hayo, Uwanja wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu, Chang'ombe wakati wa mchezo huo wa Nusu Fainali ya NSSF kati ya Jambo Leo, 'Wagumu Stars na TBC. 

Mwalimu wa TBC, Malyo Cheto, akiwapatia maelezo wachezaji wa timu hiyo, wakati wa mchezo huo, Dar es Salaam jana.

Mwalimu wa TBC, Malyo Cheto, akisisitiza jambo, wakati wa mchezo huo.

Mkurugenzi wa Jambo Concepts, inayochapisha magazeti ya Jambo Leo, Jambo Brand, Staa Spoti na Dar Metro, Juma Pinto, akitoa maelekezo kwa wachezaji wa Jmbo Leo wakati wa mapumziko kabla kuanza kipindi cha pili cha mchezo huo.

Mwalimu Msaidizi wa Jambo Leo, Abdul Kipenka, akitoa maelekezo kwa wachezaji wa Jambo Leo, wakati wa mapumziko.


Wachezaji wa timu ya Netiboli ya Jambo Leo, wakiongozwa na Mwalimu wao, Bi. Amina Kindemile (aliyekaa kushoto), wakifuatilia mchezo kati ya Kaka zao, Jambo Staa na TBC jana.


Mkurugenzi Mkuu wa www.bayana.blogspot.com, Kassim Mbarouk, hapa anaonekana akipasha tayari kwa kuchukua nafasi katika mchezo huo, kwa timu yake ya Jambo Leo, ambayo iliishinda TBC, mabao 2-0. (Picha na Ebeny-Ezary Mende)

Mchezaji Mohammed Akida, akiwaongoza wachezaji wenzake wa Jambo Leo, kuomba dua mara baada ya kumalizika mchezo huo, uwanjani hapo jana. 

Dua ikiwa imekolea, wachezaji wakiomba dua nzito kwa ajili ya mchezo ujao wa Fainali kati ya timu hiyo na Changamoto FC, mchezo utakaofanyika keshokutwa, Jumamosi, Uwanja wa Sigara (TCC), Chang'ombe, jijini Dar es Salaam nyakati za asubuhi. 

Wachezaji wa Jambo Leo na wa TBC pamoja na viongozi wao wakipiga picha ya kumbukumbu.

Kocha Msaidizi wa TBC, Swedi Mwinyi akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu hiyo,  baada ya mchezo na Jambo Stars kumalizika kwa ajili ya kujitayarisha na mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kati ya timu hiyo na IPP, mchezo utakaochezwa kesho jioni Viwanja vya Sigara, Chang'ombe.

Mwalimu Msaidizi wa Jambo Leo, Abdul Kipenka, akiwaelezea jambo, wachezaji wa Jambo Leo, baada ya mchezo kumalizika ikiwa ni matayarisho ya maandalizi ya mchezo wa Fainali kati ya timu hiyo na Changamoto FC, mchezo utakaopigwa keshokutwa Uwanja wa TCC, Chang'ombe.

Meneja wa timu ya TBC, Chacha Maginga akiwaeleza jambo wachezaji wa timu hiyo,  baada ya mchezo na Jambo Stars kumalizika, ikiwa ni katika mipango ya maandalizi ya mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kati ya timu hiyo na IPP, mchezo utakaochezwa kesho jioni Viwanja vya Sigara, Chang'ombe.

No comments:

Post a Comment