TANGAZO


Tuesday, March 19, 2013

Azam FC yawasili jijini Dar es Salaam yapata mapokezi ya nguvu


Baadhi ya wachezaji wa Azam FC wakiwasili nchini, wakitokea nchini Liberia walikokwenda kwa ajili ya mchezo wao wa kuiwakilisha Tanzania katika Kombe la Shirikisho (CAF), nchini humo, walikopambana na timu ya Barrack Young Controllers (BYC) na kuichapa mabao 2-1.

 
 Mwaikimba akiwa na baadhi ya wachezaji wenzake walipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo asubuhi.

Na Mroki Mroki wa Father Kidevu Blog-DSM
WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika (CAF), wamerejea jijini Dar es Salaam leo na kupokelewa kwa shangwe na mashabiki pamoja na wapenzi wa timu hiyo,  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Azam waliwasilini kwa mafungu kwa ndege ya Kenya Airways, ambapo baadhi ya wachezaji wakiwapo wanaoichezea timu ya Taifa, Taifa Stars kubaki Nairobi ispokuwa Mcha Khamis.

Azam FC, ambao msimu huu wapo nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, walikuwa nchini Liberia kuchuana na timu ya  Barrack Young Controllers (BYC), ambapo Azam FC, waliitandika mabao 2-1 katika mchezo huo wa kwanza wa raundi ya pili ya michuano hiyo, uliofanyika Uwanja wa Antonette Tubman jijini Monrovia, Liberia.

Azam sasa itahitaji sare tu, ili kusonga mbele katika michuano hiyo na kuingia raundi ya tatu na ya mwisho ya mchujo kabla ya hatua ya makundi.


 Pichani ni baadhi ya wachezaji hao walipowasili uwanjani hapo leo asubuhi.

Baadhi ya mashabiki na wapenzi wa timu ya Azam 
FC, wakicheza ngoma kutokana na furaha, wakati wa mapokezi ya timu hiyo leo asubuhi.


Mmoja wa mashabiki wa timu hiyo, akionesha jezi yenye maneno ya kejeli kwa timu kubwa za Simba na Yanga, zote za jijini Dar es Salaam.
SIMBA, YANGA ZILILIPENDWA... hivi ndivyo shabiki huyu wa Azam FC alivyoandika jezi yake na akitoa salamu kwa Watani hao wa jadi katika soka nchini.

Wachezaji wa Azam FC wakipanda basi lao.

No comments:

Post a Comment