TANGAZO


Tuesday, February 12, 2013

Waziri Mkuu Mizengo Pinda, azindua jengo jipya lenye mashine za kisasa la Taasisi ya Saratani, Ocean Road jijini Dar es Salaam

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda (katikati), akikata utepe kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA), Yukiya Amano (wa pili kushoto), kuashiria uzinduzi rasmi wa jengo jipya lenye vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa kansa katika Taasisi ya Kansa, Ocean Road, jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Profesa Twalib Ngoma (wa tatu kushoto) na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid. (Picha zote na Aron Msigwa – MAELEZO)
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda (katikati), akiwaonesha wageni mbalimbali, waliohudhuria uzinduzi wa jengo jipya la kuwahudumia wagonjwa wa kansa  katika Hospitali ya Kansa ya Ocean Road,  jijini Dar es Salaam leo, kitabu cha Mkakati wa Kitaifa wa Kudhibiti na Kupambana na Kansa nchini.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam leo, mara baada ya kuzindua jengo jipya la Taasisi ya Kansa, Ocean Road, lililojengwa na Serikali ya Tanzania, lenye uwezo wa kuhudumia wagonjwa 257 kwa gharama ya shilingi bilioni 7.2, huku Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA), likichangia mashine 2 za kutambua sehemu zilizoathiriwa na ugonjwa wa kansa katika mwili wa binadamu, zenye uwezo wa kuhudumia wagonjwa 1600 kila moja kwa mwaka.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki  Duniani (IAEA), Yukiya Amano, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam leo, mara baada ya kuzinduliwa kwa jengo jipya la Taasisi ya Kansa, Ocean Road jijini na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia), lililojengwa na Serikali ya Tanzania huku shirika hilo, likitoa msaada wa mashine 2 za kutambua athari za ugonjwa wa kansa kwenye mwili wa binadamu.
Baadhi ya Wataalam wa Taasisi ya Kansa ya Ocean Road, wakiwa ndani ya moja ya chumba cha  jengo jipya, lililozinduliwa jijini Dar es Salaam leo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (hayupo pichani), chenye moja ya mashine yenye uwezo wa kuwahudumia wagonjwa 1600 kwa mwaka. Mashine hiyo, imetolewa na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA).
Sehemu ya nje ya jengo jipya la Taasisi ya Kansa ya Ocean Road, lenye vifaa vya kisasa lilozinduliwa leo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, jijini  Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment