Pages

Thursday, February 7, 2013

Rais Kikwete azindua utoaji Vitambulisho vya Taifa, Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akibonyesha kitufe kuashiria kuzindua rasmi mfumo wa usajili na utambuzi wa watu na utoaji wa vitambulisho vya Taifa, uliofanyika katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam leo. Wa tatu kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, wa kwanza ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Mwaimu na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik. (Picha  zote na Freddy Maro)
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, wakiangalia bango lenye kitambulisho cha  taifa cha Rais Kikwete, muda mfupi baada ya Rais kuzindua mfumo wa usajili na utambuzi wa watu na utoaji wa Vitambulisho vya Taifa, uliofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akimkabidhi Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Kitambukisho cha Taifa katika hafla, iliyofanyika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akimkabidhi mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, kitambulisho chake cha Taifa katika viwanja vya Karimjee leo, huku Rais Kikwete akishuhudia. Kushoto ni  Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Mwaimu.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkabidhi Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi kitambulisho chake cha taifa katika viwanja vya Karimjee leo, jijini Dar es Salaam.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkabidhi Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa kitambulisho chake cha taifa katika viwanja vya Karimjee leo.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkabidhi Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kitambulisho chake cha taifa katika viwanja vya Karimjee leo.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad kitambilisho chake cha Taifa katika viwanja vya Karimjee leo, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa usajili na utambuzi wa watu.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkabidhi Askofu Malasusa wa KKKT, kitambulisho chake cha Taifa.
Rais Kikwete, akimkabidhi kada wa CCM, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, kitambulisho chake cha Taifa.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkabidhi Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Elihad Salum, kitambulisho cha Taifa.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba kitambukisho chake cha Taifa, wakati wa uzinduzi huo.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau kitambulisho chake cha Taifa leo, katika viwanja vya Karimjee.
Rais Dk. Jakaya Kikwete, akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Eriyo, kitambulisho chake cha Taifa. 

No comments:

Post a Comment