Pages

Sunday, February 10, 2013

Rais Kikwete akabidhi Bajaj kwa mlemavu, afungua Semina ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Dodoma

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkabidhi Bajaji mpya mlemavu wa miguu ambaye ni mfanyakazi wa TANROADS, Sarah Nalingigwa Nkumbo huko Ikulu, mjini Dodoma leo asubuhi. Bi. Sarah ambaye ni Mfanyakazi wa TANROADS mkoani Singida alikabidhiwa Bajaji hiyo, ikiwa ni ahadi ya Rais alipokuwa akifungua Barabara ya Manyoni- Itigi. (Picha zote na Freddy Maro)
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi funguo ya Bajaji mpya, mlemavu wa miguu ambaye ni mfanyakazi wa TANROADS, Sarah Nalingigwa Nkumbo huko, Ikulu mjini Dodoma leo asubuhi. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, John Pombe Magufuli. Bi. Sarah ambaye ni Mfanyakazi wa TANROADS mkoani Singida, alikabidhiwa Bajaji hiyo, ikiwa ni ahadi ya Rais alipokuwa akifungua Barabara ya Manyoni- Itigi. 

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mlemavu wa miguu, ambaye ni mfanyakazi wa TANROADS, Sarah Nalingigwa Nkumbo (aliyekaa), huko Ikulu mjini Dodoma leo asubuhi. Kulia ni Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli, wa pili kushoto ni mke wa Rais, Mama Salma Kikwete na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TANROADS, Injinia Patrick Mfugale. Bi. Sarah ambaye ni Mfanyakazi wa TANROADS mkoani Singida, alikabidhiwa Bajaji hiyo, ikiwa ni ahadi ya Rais alipokuwa akifungua Barabara ya Manyoni- Itigi. 

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mlemavu wa miguu ambaye ni mfanyakazi wa TANROADS, Sarah Nalingigwa Nkumbo baada ya kumkabidhi Bajaji mpya, huko Ikulu, mjini Dodoma leo asubuhi. Kulia ni Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli, wapili kushoto ni mke wa Rais, Mama Salma Kikwete na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TANROADS, Injinia Patrick Mfugale. Bi. Sarah ambaye ni Mfanyakazi wa TANROADS mkoani Singida alikabidhiwa Bajaji hiyo, ikiwa ni ahadi ya Rais alipokuwa akifungua Barabara ya Manyoni- Itigi. 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula (kushoto) na Katibu Mkuu wa CCM, Abdurrahman Kinana, wakiingia katika ukumbi wa mikutano wa White House, uliopo Makao Makuu ya chama hicho, mjini Dodoma leo. Rais Kikwete amefungua na kuongoza semina kwaajili ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambayo pamoja na mambo mengine itachagua wajumbe wa Kamati Kuu.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, wakiwa katika semina maalum, iliyofunguliwa na kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, ukumbi wa White House, Makao Makuu ya chama hicho, mjini Dodoma leo.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akielekeza jambo, wakati alipokuwa akiifungua Semina maalum kwa ajili ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Taifa, iliyofanyika mjini Dodoma, ukumbi wa White House Makao Makuu leo. Kushoto anayesikiliza kwa makini ni Makamu  Mwenyekiti mstaafu wa CCM Bara, Pius Msekwa. Wengine katika picha ni Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (wapili kushoto), Katibu Mkuu, Abdurrahman Kinana (wanne) na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara,  Philip Mangula.


Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza wakati alipokuwa akiifungua Semina maalum kwa ajili ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Taifa, iliyofanyika mjini Dodoma, ukumbi wa White House Makao Makuu leo. Kutoka kushoto ni Makamu  Mwenyekiti mstaafu wa CCM Bara, Pius Msekwa, Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, Katibu Mkuu, Abdurrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara,  Philip Mangula.

No comments:

Post a Comment