Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NMB, Imani Kajula akipokea Tuzo ya Superbrands kutoka kwa Mkurugenzi wa Superbrands Afrika Mashariki, Jawad Jaffer wakati wa hafla za kuwakabidhi washindi wa tuzo hizo ambapo benki ya NMB, imekua mshindi katika Taasisi za Kifedha nchini.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB, Mark Wiessing (katikati) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Imani Kajula (kushoto) na Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga, wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo ya Superbrands jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB, Mark Wiessing (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Imani Kajula, wakifuatilia utoaji huo wa tuzo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa benki ya NMB Imani Kajula, akizungumza jambo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Mark Wiessing, wakati wa hafla hiyo, ambayo NMB, imeibuka kinara wa tuzo hizo kwa sekta za kibenki.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB, Mark Wiessing (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Imani Kajula (kushoto), wakimsikiliza Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga, wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo ya Superbrands jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote kwa hisani ya Habari Mseto Blog)
DAR ES SALAAM, Tanzania
BENKI ya NMB imeibuka kinara wa tuzo za Ubora wa Makampuni ‘Superbrands 2013/14’ kwa upande wa Taasisi za Kifedha nchini, huku ikiahidi kuboresha utendaji wao na sasa wateja watapata huduma popote walipo bila kwenda kwenye matawi ya benki hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, wakati wa hafla ya kupokea tuzo hiyo, kutoka kwa Mkurugenzi wa Superbrands, Afrika Mashariki, Jawad Jaffer, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa NMB, Iman Kajula alisema kwao ni zaidi ya fahari kwa kuwa kinara wa Superbrands kwenye sekta ya fedha.
Ushindani wa katika taasisi za kifedha, nia ya dhati ya kusadia ukuzaji maendeleo kwa wateja wake na kuendelea kuwa kinara wa miongoni mwa makampuni bora kwa huduma, yanaisukuma NMB kuhamishia huduma za kibenki katika simu za mikononi za wateja wao na Watanzania kwa ujumla.
“NMB inajisikia fahari kubwa kuwa kinara wa ‘Superbrands’ katika sekta ya fedha na ili kujiweka juu zaidi, tumepania kupunguza msongamano kwenye matawi yetu kwa kuhamishia huduma za kibeki katika simu na kuharakisha harakati chanya za maendeleo,” alisema Kajula.
Aliongeza kuwa, kwa miaka sita sasa NMB imepanua wigo wa maendeleo yake na wateja kwa ujumla, ambapo kwa sasa ina zaidi ya matawi 148, ATM 500, wakiwamo pia wateja wanaotumia simu za mkononi ‘NMB Mobile’ zaidi ya 800,000 na huduma mbadala kama Internet Banking Call Center.
No comments:
Post a Comment