Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa nchini, Abbas Kandoro, akihutubia mjini Mtwara leo, wakati alipokuwa akilifunga Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Wanahabari, kujadili utafiti uliofanywa na wanahabari kuhusu matumizi ya fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajili ya afya katika Halmashauri 26 nchini. Kongamano hilo, lilifanyika kwa siku mbili, Chuo cha Ualimu mkoani Mtwara.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akielezea jinsi ya kuwaomba watabibu kutoka wizarani kwenda kwenye Halmashauri mbalimbali nchini pamoja na Hospitali. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba, akizungumza katika ufungaji wa kongamano hilo, kwa kuwapongeza wanahabari waliofanya utafiti huo.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, akihutubia na kushukuru kwa kongamano hilo, kufanyika wilayani humo. |
Mwenyekiti wa Kongamano hilo, John Bwire akiendesha mijadala mbalimbali, kabla ya kufungwa kongamano hilo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro leo.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Raphael Mwamotto, akielezea katika kongamano hilo, jinsi wanavyowabaini wanachama walaghai.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NHIF, Eugen Mikongoto (kulia), akiwa katika kikao na baadhi ya Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakuu wa baadhi ya Mikoa ili kuweka mambo sawa. |
Mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe, Sharon Sauwa, akiwasilisha utafiti wake katika kongamano hilo kala ya kufungwa kwake leo, mjini Mtwara.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba (kushoto), akijadili jambo na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid katika kongamano hilo.
Wanahabari Celina Wilson wa Uhuru na Tausi Mbowe wa Mwananchi, wakiwa katika Kongamano hilo.
|
Mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Dar es Salaam, Faraja Kihongole (kushoto), akiwa na mwenzie Vivian kutoka Kigoma kwenye kongamano hilo. |
Wanahabari wakiwa kazini wakati wa kongamano hilo.
Ofisa Mahusiano wa NHIF, Grace Kisinga (kulia) na mwenzie wakiwajibika wakati wa kongamano hilo, kuhakikisha mambo yanakwenda sawia.
Baadhi ya Wakurugenzi na Maofisa wa NHIF, wakisikiliza kwa makini mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiendelea katika kongamano hilo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani, akielezea kuhusu utendaji wa Bohari hiyo, pamoja na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo.
|
No comments:
Post a Comment