|
Polisi wakiwa katika doria kuhakikisha maandamano ya Chama cha Wananchi (CUF), hayafanyiki mjini Lindi jana. |
|
Safari ya doria ilianzia hapa kwenye eneo la Kituo Cha Polisi, mjini Lindi. |
|
Gari la doria ya Polisi ikiwa kwenye kituo cha mabasi, mjini Lindi. |
|
Mwenyekiti wa CUF, wilaya ya Lindi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini, Salum Barwany, akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani), mjini Lindi kuhusu maandamano hayo. |
|
Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, George Mwakajinga akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani), kuhusu sababu za kusitishwa maandamano hayo.
|
KUSITISHSHWA kwa maandamano hayo, kunafuatia barua ya Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Lindi, ya tarehe 20, mwezi huu kwa Chama hicho, cha CUF kuyakataa maombi yao ya kutaka kufanya maandamano makubwa na mkutano wa hadhara.
Katika barua hiyo, CUF, ilitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi Wilaya ya Lindi ya kutaka kufanya maandamano makubwa na mkutano wa hadhara kwa lengo la kuishinikiza Serikali kutoa tathmini ya Maendeleo ya Miradi ya Gesi asilia, Maji, Stakabadhi ghalani pamoja kupatiwa taarifa ya kuanza kutekelezwa kwa ahadi za Serikali juu ya ujenzi wa viwanda vitavyotokana na gesi na kuitafsiri mikataba ya gesi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na suala hilo la maandamano, Mbunge wa chama hicho, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wilaya, Salum Barwany, amesema chama chake kimelazimika kusitisha maandamano hayo kwa muda hadi tarehe 03, mwezi ujao na kusisitiza kwamba maandamano ni haki ya msingi kuwawezesha wananchi kutoa kero zao.
Sambamba na hilo, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Lindi, George Mwakajinga, ameeleza kuwa Ofisi yake imeamua kuzuia maandamano hayo, kufuatia mialiko mbalimbali iliyotolewa kwa mkoa wa Mtwara ambako hivi karibuni kulitokea hali ya uvunjifu wa amani na kusababisha vifo, uchomaji wa moto kwa nyumba za Wabunge na Serikali, yakiwemo magari.
‘’Maandamano ni haki ya msingi kwa vyama vya siasa, ila inatushangaza unapotoa mialiko kwa mikoa mingine, hii imetuweka njia panda, inakuwaje maandamano ya Lindi, waje na Mtwara, hii hapana ni lazima Jeshi lijipange, ndiyo tutaruhusu kwa kuwa tetesi tulizozipata wengine wanakuja kwa ajili ya fujo," alimalizia Kamanda Mwakajinga.
No comments:
Post a Comment