TANGAZO


Tuesday, February 12, 2013

EfG yaendesha semina ya Mjadala wa kuweka mikakati ya kuondoa Ukatili wa Kijinsia katika Masoko ya Ilala jijini Dar es Salaam

Ofisa wa Jeshi la Polisi, mwenye cheo cha Sajenti, Dorice Gweba kutoka Wilaya ya Ilala, ambaye anashughulika na Dawati la Kupokea  Matukio  ya Kijinsia, akitoa mada katika semina ya mjadala  wa kuweka mikakati ya kuondoa ukatili wa kijinsia  katika Masoko ya Manispaa ya Ilala. Mjadala huo, uliandaliwa na  Shirika lisilo la Kiserikali la Equality for Growth (EfG), Dar es Salaam leo. (Picha zote na mwaibale.blogspot.com)
Sajenti Dorice Gweba, akitoa ufafanuzi kwa wajasiriamali wanawake kutoogopa mkuripoti Polisi baada ya kufanyiwa ukati wa kijinsia katika masoko wanayofanyia biashara.
Mwezeshaji wa semina hiyo Frank Chambua (kushoto), akichambua mada katika semina hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la  Equality for Growth (EfG), Jane Magigita (kulia),  akifafanua jambo kwa msisitizo katika semina hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la  Equality for Growth (EfG), Jane Magigita  (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari.
Mjasiriamali katika soko la Samaki la Feri, Hilda Mtelemwa, akitoa ushuhudi 
wa ukatili wa jinsia aliowahi kufanyiwa.
Viongozi wa kamati za masoko ya Manispaa ya Ilala wakiwa kwenye semina hiyo.
Maofisa wa EfG, wakiwa katika meza yao ya uwajibikaji. Kushoto ni Evah Buhembo na Noera Lema.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye semina hiyo.
Wenyeviti wa masoko ya Manispaa ya Ilala wakiwa katika semina hiyo.
Waandishi wa habari wakifuatilia matukio mbalimbali katika semina hiyo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye semina hiyo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye semina hiyo.

No comments:

Post a Comment