TANGAZO


Wednesday, January 16, 2013

18 wanusurika kufa kwa moto Soko Muhogo, Mjini Zanzibar


Wananchi wakisaidia kuzima moto huo.
Vitu vilivyoteketea kwa moto kwenye stoo, ambako kulikuwa na mita ya umeme pamoja na jiko la umeme ambalo wakazi wa nyumba hiyo wamedai kutolitumia jiko hilo..
Viongozi wa Shehia ya Shangani wakiangalia halihalisi ya tukio hilo la mototo. (Picha na maelezo na Martin Kabemba)

WATU 18 wa familia 4 ya Imtiaz Kassim Yakub Dada, wamenusurika kifo katika janga la moto uliotokea jana saa 5 asubuhi kwenye nyumba namba 424, mtaa wa Sokomhogo, Mjimkongwe wa Zanzibar.

Moto huo, ambao chanzo chake hakijajulikana, ulianzia kwenye stoo na kuteketeza vitu vilivyokuwa vimehifadhiwa humo ambavyo thaani yake bado kujulikana. moto huo, ulizimwa mapema kwa msaada wa  Hoteli ya Marumaru ya mjini Zanzibar muda mfupi kabla ya Zimamoto kuwasili kwenye tukio hilo.

Zimamoto, wametoa pongezi kwa uongozi wa Hoteli hiyo, chini ya Meneja wake Mkuu, Prithvi Olivier Spears kwa kutoa  huduma  ya kwanza huku wakitumia vifaa vyao vya hoteli.

No comments:

Post a Comment