TANGAZO


Thursday, December 20, 2012

Matokeo darasa la Saba yatolewa, Waziri Dk. Kawambwa asema ufaulu umeongezeka

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akitoa taarifa ya matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (darasa la Saba), mwaka 2012. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, wakati alipokuwa akitoa taarifa ya matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (darasa la Saba), mwaka 2012.
 
Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza nao, Dar es Salaam leo, alipokuwa akitoa taarifa ya matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (darasa la Saba), mwaka 2012.
 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (darasa la Saba), mwaka 2012. Kulia ni Kamishna wa Elimu, wizarani hapo, Profesa Eustella Bhalalusesa.
 



Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza nao, Dar es Salaam leo, alipokuwa akitoa taarifa ya matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (darasa la Saba), mwaka 2012.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, akijibu maswali ya waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akizungumza nao, alipokuwa akitoa taarifa ya matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (darasa la Saba), mwaka 2012. Kulia ni Kamishna wa Elimu, wizarani hapo, Profesa Eustella Bhalalusesa.
 
 
Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
Disemba 20, 2012
JUMLA ya wanafunzi 560,706 kati ya 865,534, waliofanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi mwaka huu, wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani, huku hali ya udanganyifu ikionekana kushuka kulinganishwa na mwaka jana.
 
Akitoa matokeo ya mtihani huo leo, jijini Dar es Salaam, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, alisema kwamba wanafunzi hao, wamefaulu kujiunga na shule za Sekondari za Serikali kwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2013.
 
Dk. Kawambwa alisema kwamba kati ya wanafunzi hao, waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza, wasichana wanaongoza kwa kuwa na idadi 281,460, sawa na asilimia 50.20 huku wavulana wakiwa 279,246, sawa na asilimia 49.80.
 
Kwa mujibu wa Dk. Kawambwa ufaulu huo, umepanda kwa asilimia 8.8 kulinganishwa na mwaka 2011 ambapo wanafunzi 515,187 pekee ndio waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.
 
Kuhusiana na kupungua kwa idadi ya wanafunzi waliofanya udanganyifu, Dk. Kawambwa alisema idadi ya wanafunzi hao, imeshuka na kwamba Serikali imewafutia matokeo watahiniwa 293 kulinganisha na 9,736 waliofutiwa mwaka jana.
 
"Kwa mwaka huu, mafanikio moja wapo ni kupungua kwa idadi ya watahiniwa waliofanya udanganyifu, Serikali imebaini kuwapo watahiniwa 293, waliofanya udanganyifu kulinganishwa na idadi ya mwaka jana waliokuwa 9,736 na hao watachukuliwa hatua stahiki"alisema Dk. Kawambwa.
 
Kuhusiana na teknolojia mpya iliyotumika ya kusahihisha mtihani huyo kwa mfumo wa kompyuta, Dk. Kawambwa alisema kwamba imeleta mafanikio hasa kutumia muda mchache kusahihisha kulinganishwa na miaka mingine iliyopita.
 
Alisema kuwa kwa mwaka huu Serikali imetumia walimu 200 kusahihisha mitihani hiyo kwa mfumo maalimu wa kompyuta, kulinganishwa na mwaka jana ambapo ilitumia walimu zaidi ya 4,000 kusahihisha mitihani hiyo.
 
Aliongeza kuwa mbali na kutumia idadi ndogo ya walimu kusahihisha, pia imeweza kusahihisha mitihani hiyo kwa siku 15 kulinganishwa na miaka mingine ambapo iliilazimu kutumia zaidi ya mwezi mmoja kusahihisha.
 
Dk Kawambwa alisema kwamba jumla ya wanafunzi 865,827 kati ya 894,839 walioandikishwa kufanya mtihani huo, waliofanya mtihani kwa kutumia teknolojia mpya ya OMR.
 
Alisema kwamba mfumo huo mpya wa OMR ambao unamlazimu mwanafunzi kuchagua jibu sahihi katika maswali yake, umekwenda vizuri ikiwa ni mara ya kwanza kuanza kutumika hapa nchini.
 

No comments:

Post a Comment