Mchezaji Mgaya Jaffari wa Azam FC, akiutoa mpira miguuni mwa Abdi Banda wa Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Fainali ya Uhai Cup, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam leo.
Hussein Juma wa Coastal Union akikimbia mpira kuelekea langoni mwa timu ya Azam FC katika mchezo huo.
Hussein Juma wa Coastal Union akijaribu kukwepa kwanja la Jaffari Mgaya (kushoto) wa Azam FC katika mchezo huo.
Mashabiki wakifuatilia mchezo wa fainali, uliokuwa wa vuta nikuvute kati ya timu ya Azam FC na Coastal Union ya Tanga, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam leo.
Meza kuu, iliyokuwa na viongozi mbalimbali wa ngazi ya juu wa TFF, wakifuatilia mchezo huo wa fainali, uliokuwa wa vuta nikuvute kati ya timu ya Azam FC na Coastal Union ya Tanga, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam leo.
Meza kuu, iliyokuwa na viongozi mbalimbali wa ngazi ya juu wa TFF, wakifurahia moja ya vitendo vya kufurahisha vilivyokuwa vikifanywa na wachezaji wa timu hizo katika mchezo huo wa fainali, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam leo.
Wachezaji wa Coastal Union wakifurahiya bao la pili la timu hiyo dhidi ya Azam FC, ambalo lilikuwa la kusawazisha na hivyo timu hizo kumaliza dakika 90 zikiwa nguvu sawa na kisha kuongezwa nyingine 30, ambapo pia zilishindwa kufungana, hadi zilipopigiana penalti tano tano na hivyo Azam FC ikashinda kwa mikwaju 3-1.
Mashabiki wa Coastal Union wakishangilia bao la kusawazisha la timu hiyo dhidi ya Azam FC.
Hussein Juma (kushoto) wa Coastal Union, akitafuta mbinu ya kumtoka Samwel Nkomola wa Azam FC katika mchezo huo.
Mashabiki waliokuwa wamejazana wakifuatilia mchezo wa fainali kati ya timu hizo, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam leo jioni.
Hussein Juma (kushoto) wa Coastal Union na Samwel Nkomola wa Azam FC, wakikimbilia mpira katika mchezo huo.
Hussein Juma (kushoto) wa Coastal Union na Samwel Nkomola wa Azam FC, wakikimbilia mpira wakati wa mpambano wa fainali ya michuano ya Uhai Cup, Uwanja wa Karume jijini leo.
Hussein Juma (kushoto) wa Coastal Union na Samwel Nkomola wa Azam FC, wakiwania mpira uliokuwa katikaati yao, wakati wa mchezo huo.
Golikipa wa Azam FC, akipangua penalti ya mwisho ya timu ya Vijana wa Coastal Union, wakati wa kupigiana penalti tano, tano.
Wachezaji wa Coastal Union wakinyanyuliwa baada ya timu yao kukosa penalti ya mwisho na hivyo, wapinzani wao, Azam FC, wakatawazwa kuwa mabingwa wa Uhai Cup 2012, Uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti na Mkurugenzi wa timu za Azam, akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali wa michuano hiyo.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Leodeger Tenga, akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali wa michuano hiyo.
Baadhi ya wachezaji wa Azam FC, mabingwa wapya wa Uhai Cup, wakiwa wamekaa chini wakisikiliza mambo mbalimbali yaliyokuwa yakizungumzwa na viongozi wa TFF.
Refa bora wa michuano hiyo, akikabidhiwa kikombe chake na fedha taslim wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa michuano hiyo.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodeger Tenga, akiwavalisha medali za dhahabu wachezaji wa Azam FC baada ya kuifunga timu ya Vijana wa Coastal Union kwa penalti 3-1 baada ya kufungana mabao 2-2 katika dakika 120 za mchezo huo.
Mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Kanali mstaafu Idd Kipingu (kulia), akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa mashindano ya Uhai Cup, Nahodha wa timu ya Azam FC, Abdul Mgaya baada ya timu hiyo kuwashinda vijana ya Coastal Union kwa mikwaju ya penalti 3-1 baada kumaliza dakika 120 zikiwa sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam leo. Katikati ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodeger Tenga.
No comments:
Post a Comment