TANGAZO


Saturday, December 22, 2012

Taifa Stars yawalaza bingwa wa Afrika, Chipolopolo ya Zambia, yaipiga 1-0 Uwanja wa Taifa

 

Wachezaji wa Taifa Stars wakimpongeza Mrisho Ngassa baada ya kuipatia Stars bao la kuongoza dhidi ya timu ya Taifa ya Zambia (Chipolopolo) katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa uliochezwa leo, Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Taifa Stars imeshinda bao 1-0.
 
Mashabiki wa Stars wakifuatilia mchezo huo.
 
Mchezaji Mwinyi Kazimoto wa Taifa Stars, akimtoka Sululan Phiri wa timu ya Taifa ya Zambia 'Chipolopolo' katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
 
TAIFA Stars leo, imetoka kifua mbele kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Zambia 'Chipolopolo', lililopatikana dakika ya 45 ya mchezo. Bao hilo limefungwa na mchezaji Mrisho Ngassa, kwa shuti la mbali akimalizia pasi ya Mwinyi Kazi moto.

Bao hilo la aina yake, lilidumu hadi kipenga cha mwisho, lilifungwa umbali yapata kama mita 18 hivi likimwacha golikipa wa timu hiyo akiruka bila mafanikio.

Katika kipindi hicho kila timu iliweza kufanya mashambulizi makali lakini safu ya ushambuliaji ya Stars ilishindwa kujiamini kwa kupoteza mipira mingi iliyokuwa inaipata pembeni mwa lango la Chipolopolo.

Hata hivyo, Zambia haikuonesha sana makeke kama ilivyo kwa Stars kupitia kwa mchezaji wake Ngassa ambaye alikuwa akipoteza mpira mingi kwa kutokuwa makini kwa kuogopa kufanyiwa rafu.

Stars-Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Kelvin Nyondani,Frank Domayo,Amir Kiemba,Salum Abubakar,Mrisho Ngassa,Mwinyi Kazimoto, Hamis Mcha/Simon Msuva.

Zambia- Danny Munyao, Chintui Kapamba,Hichani Himonde,Chisamba Lungu,Jame Chamanga/Shadrack
Malambo,Christopher Katondo/Stoppila Sunzu,Felix Katongo,Nathan Sinkala/Evans Kangwa,Roderick Kabwe/Francis Kasonde na Issac Chansa.

No comments:

Post a Comment