TANGAZO


Saturday, December 29, 2012

Simba yakubali 3-0 mbele ya Tusker ya Kenya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Mchezaji Abdallah Juma wa Simba, akizuia mpira huku akikabwa na Mark Odhiambo wa Tusker ya Kinya wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Tusker imeshinda mabao 3-0. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

 Kiggi Makassy wa Simba (kushoto), akikimbilia mpira na Jeremiah Bright wa Tusker.

 Kiggi Makassy wa Simba (kushoto), na Jeremiah Bright wa Tusker, wakikimbilia mpira.

 Kiggi Makassy wa Simba, akipiga mpira mbele ya Jeremiah Bright wa Tusker.

Mussa Mude wa Simba (kushoto), akimtoka Jeremiah Bright wa Tusker, anayejaribu kuutoa mpira miguuni mwake.

Mussa Mude wa Simba, akitafuta mbinu ya kumtoka Jeremiah Bright wa Tusker wakati wa mchezo huo.

Mussa Mude wa Simba, akimhadaa Jeremiah Bright wa Tusker.

 Mussa Mude wa Simba na Jeremiah Bright wa Tusker, wakisigana katika mchezo huo.

  Mussa Mude wa Simba na Jeremiah Bright wa Tusker.

 Mashabiki wa Simba, wakifuatilia mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es salaam leo jioni.

 Haruna Moshi 'Boban' wa Simba, akichuana na Martin Kiiza wa Tusker.

Zikiwa dakika zimeshayoyoma bado Simba hawakuweza kupata hata bao la kufutia machozi kama ilivyokuwa ikionekana kwenye ubao wa matangazo.

 Mussa Mude wa Simba, akitafuta mbinu ya kumtoka Martin Kiiza wa Tusker.

 Maurice Odipo wa Tusker, akimpiga kwanja Harun Athuman wa Simba.

 Jonas mkude wa Simba (kulia), akikimbilia mpira na Mark Odhiambo wa Tusker.



Jonas Mkude wa Simba (kulia), akitafuta mbinu ya kumtoka Humphrey Okoth wa Tusker.

Wachezaji wa Simba na Tusker, wakitoka uwanjani baada ya kukusanyika pamoja na kuomba dua ya pamoja.

Wachezaji wa Simba na Tusker, wakitoka uwanjani baada ya kumalizika kwa mchezo na Tusker kutoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 3-0.

No comments:

Post a Comment