TANGAZO


Sunday, December 23, 2012

Sherehe za Mahafali ya 10 ya Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), jijini Dar es Salaam



Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa jengo jipya la Utawala la Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), Barabara ya Kilwa Dar es Salaam jana, Desemba 22 -2012.
Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya (katikati), akiwa mbele ya jengo hilo, baada ya kulifungua rasmi. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo hicho, Profesa Isaya Jairo na Mtendaji Mkuu wa Chuo hicho, Shah Hanzuruni.
Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya (katikati), akiwa na viongozi mbalimbali na wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania baada ya kulifungua jengo la utawala.
Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya (katikati), akienda kujiandaa kwa mahafali hayo, baada ya kufungua jengo jipya la utawala. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Shah Hanzuruni na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi hiyo, Profesa Isaya Jairo .
Wahadhiri wa Taasisi hiyo, wakiandamana kwenda uwanjani tayari kwa hafla hiyo.
Wakufunzi wa Taasisi hiyo wakienda uwanjani katika mahafali hayo.
Wapiga picha wakichukua matukio mbalimbali ya mahafali hayo.
Kikosi cha band cha Jeshi la Magereza kikiongoza maandamano kuelekea uwanjani kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wa fani ya uhasibu wakiwa katika mahafali hayo.
Wahitimu wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), wakiwa katika mahafali yao hayo.
Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya (katikati), ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 10 ya Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), akiwa meza  kuu na viongozi wengine wakati wimbo wa Taifa ulipokuwa ukipigwa kabla ya kuanza kwa sherehe hizo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya Uhasibu Tanzania (NBAA), Pius Maneno, Menyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Isaya Jairo, Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Shah Hanzuruni na Dk.Judica King'ori.
Wahitimu wakiwa katika mahafali yao hayo.
Wahitmu wakitunukiwa shahada zao wakati wa mahafali yao hayo.
Baadhi ya wahitmu wa Chuo hicho, wakitunukiwa shahada zao wakati wa mahafali yao hayo.
James Mponda ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Ifushilo, iliyopo Ukwavila Mbarali, mkoani Mbeya akimpongeza mkewe, Regina Chiganga kwa kumvika shada la maua baada ya kutunukiwa shahada ya kwanza ya uhasibu katika Taasisi hiyo. Regina ni Mwalimu wa Sekondari ya Mtakatifu Anthony iliyopo Mbagala Kipati, Dar es Salaam.
Mponda na mkewe, Regina wakiwa katika matukio tofauti wakifurahia hatua hiyo, nzuri katika maisha yao, hakika wanapendeza.
Mponda na akimpatia kadi mkewe, Regina mara baada ya kuhitimu chuoni hapo jana. 

Askari mgambo wakitoa saluti wakati wimbo wa Taifa ulipo kuwa ukipigwa kabla ya kuanza kwa hafla hiyo.(Picha zote kwa hisani ya mwaibale.blogspot.com)

No comments:

Post a Comment