Waziri wa Fedha, Dk. Wiliam Mgimwa akifungua mafunzo ya wajasiriamali leo, yaliyoandaliwa na Mbunge wa
viti maalum Mkoa wa Iringa (CCM), Ritta Kabati.
|
Waziri wa
Fedha, Dk. William Mgimwa, akimkabidhi Mbunge wa Viti maalum (CCM), Ritta Kabati
kiasi cha sh. milioni 1 kwa ajili ya kuchangia vikundi vya ujasiriamali mkoani humo. (Picha zote na
Denis Mlowe)
Na francisgodwin.blogspot, Denis Mlowe
Iringa, 17/12/2012
WAZIRI wa fedha
na uchumi, Dk. Wiliam Mgimwa ametangaza vita kali kwa mafisadi wanaoficha fedha
katika mabenki ya nje ya nchi.
Waziri Mgimwa, ameyasema hayo leo,
wakati akizungumza na waandishi wa mkoani Iringa mara baada ya kufungua mafunzo
ya ujasiriamali kwa vikundi 29 vilivyoko mkoani hapa vinavyofadhiliwa na Mbunge
wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi (CCM), Mkoa wa Iringa Ritta Kabati
.
"Serikali
itawashughulikia watu wote wanaoweka fedha nje ya nchi kwa njia haramu ....
inafatilia kwa karibu sana wale walioweka fedha hizo nje ya kwa nchi kwa
kuwasiliana na nchi zinazosemekana mafisadi wanaweka fedha hizo na haina hofu na
kundi au mtu wanaosemekana wanaweka fedha katika mabenki ya nje ya nchi"
Alisema kuwa
dawa ya watu hao wanaoficha fedha nje ya nchi ipo jikoni na kusema kuwa
serikali haitalala katika kuwashughulikia watu hao wa kuchukua hatua zaidi.
Hatua hiyo ya
Waziri wa Fedha kutangaza uamuzi huo imekuja huku zikiwa zimepita siku
chache toka naibu Katibu Mkuu chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema), Zitto
Kabwe kutaka Serikali kuwabana wale wote wanaoficha fedha nje ya nchi na
kutaka fedha hizo kurejeshwa nchini.
Awali akifungua
mafunzo hayo ya ujasiriamali katika ukumbi wa Orofea mjini Iringa, Dk. Mgimwa
mbali ya kuchangia kiasi cha shilingi milioni 1 kwa ajili ya kuwasaidia
wajasiriamali hao pia aliwataka wajasiriamali mkoani Iringa kutumia mafunzo
hayo katika kujiongezea kipato .
Kwa upande wake
mbunge Kabati alisema kuwa mafunzo hayo ni moja kati ya ahadi zake kwa
wajasiriamali mkoani Iringa na kuwa lengo ni kuendelea kutekeleza ahadi zake
zaidi .
Alisema kuwa
mafunzo hayo yanatolewa na taasisi ya ujasiriamali ya Decision Foundation ya
kutoka Dar es Salaam .
Hata hivyo
Kabati alisema kuwa kuwa Serikali ya CCM imeendelea kuonyesha mfano katika
uwajibikaji kwa wananchi wake na kuwa lengo ni kuona wanaendelea kuwa na
imani ya CCM na serikali yake .
"Ndugu zangu
wananchi mbali ya mafunzo haya nimeendelea kuwa jirani na wananchi wangu wa
jimbo la Iringa mjini kwa kuwawezesha vijana na kuanzisha vikundi vya benki
za wananchi mitaani (VICOBA) pamoja na kuwasaidia watu wenye makundi mbali
mbali na sitachoka kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment