Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHDEMA), Freeman Mbowe (katikati),
akiwa katika Mahakama ya Rufaa wakati wa hukumu ya rufaani ya Mbunge wa Arusha
Mjini, Godbless Lema leo, jijini Dar es Salaam.
Wakili wa Godbless Lema, Tundu Lissu
(katikati), akiwa kwenye Mahakama ya Rufaa kusikiliza huku ya rufaani hiyo.
Mbunge wa Arusha Mjini,
Godbless Lema akilakiwa na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), baada ya kushinda rufaa yake ya kupinga kuvuliwa Ubunge wa Arusha
Mjini katika Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam leo.
Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), wakiongozwa na Mbunge wa Arushja Mjini, Godbless Lema (wa tatu kulia), kuelekea Makao
Makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
Wafuasi wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakiongozwa na Mbunge wa Arushja Mjini,
Godbless Lema (anayepunga mkono), kuelekea Makao Makuu ya chama hicho. Kinondoni jijini Dar es
Salaam.
Wakili wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Tundu
Lissu wa pili kulia), akizungumza na wafuasi wa chama hicho, Makao Makuu ya Chadema, jijini Dar es
Salaam leo mara baada ya Mbunge Lema kurejeshewa ubunge wake na Mahakama ya Rufaa jijini.
Mbunge wa Ubungo John Mnyika, akizungumza na
wafuasi wa Chadema Makao Makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini leo.
Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akizungumza na wanachama wa
chama hicho, waliokusanyika Makao Makuu ya Chama hicho, jijini Dar es Salaam leo
baada ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kushinda rufaani yake ya kupinga
kuvuliwa Ubunge katika jimbo hilo.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, akizungumza na
wafuasi wa Chadema, waliokusanyika Makao Makuu ya chama hicho, Kinondoni
jijini Dar es Salaam leo, kufurahia ushindi wake wa rufaani aliyoikata Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment