TANGAZO


Monday, December 24, 2012

Abiria zaidi wanusurika kufa ajali ya basi la New Force na Fuso, eneo la Inyala Pipeline Mbeya


Zaidi ya abiria 40 waliokuwemo kwenye basi la New Force wamenusurika kufa baada ya basi hilo kugongana na lori aina ya Fuso, maeneo ya Pipeline, Inyala Mbeya. Basi la New Force lilikuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam. 
Hizi ni damu za baadhi ya abiri waliokuwemo kwenye basi hilo.
Hili ni lori aina ya Fuso, lililosababisha ajali hiyo, kwani lilikuwa likijaribu kulipita gari lingine bila ya kuangalia kama kuna gari lingine linashuka mlima na ndipo lilipokutana uso kwa uso na basi hilo.
Hii ndiyo hali halisi ya ajali hiyo, dereva wa fuso amekimbia baada ya kusababisha ajali hiyo.
Mtoto Samwelli, akisimulia jinsi ajali hiyo, ilivyotokea kwani yeye alikuwa nyuma ya dereva  wa basi hilo. Amesema kuwa yeye mkanda ndio uliomuokoa kwani mama yake aliyekuwa jirani yake hakufunga mkanda ameumia vibaya sana.

Badhi ya abilia waliokuwa kwenye basi hilo, wakisubiri usafiri mwingine toka katika kampuni ya New Force.
Baadhi ya mjeruhi wa ajali hiyo, wameruhusiwa baada ya kupata matibabu.
Mmmoja wa majeruhi wa basi hilo, akiwa hospitali kutibiwa, akizungumza na waandishi wa habari.
Baadhi ya majeruhi wakitoka hospitalini kutibiwa.

Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufani ya Mbeya, Dk. Hamfrey Kiwelu, aliyesimama amesema wamepokea majeruhi 24 na kati ya hao 17, wameruhusiwa baada ya kupata matibabu na majeruhi 7, wamelazwa hospitalini hapo, kuendelea na matibabu. 
Hili ni basi hilo, linavyoonekana baada ya kupata ajali. (Picha zote na Mbeya Yetu blog)

No comments:

Post a Comment