Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Kulinda Haki za Ubunifu (WIPO), Neema Nyerere, akizungumza katika hafla ya kutiliana saini Mkataba wa Uwekaji wa Nembo ya Karafuu ambayo itatumika katika Zao la Karafuu ya Zanzibar. kushoto ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Nassor Ahmed Mazrui na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha Biashara (ITC), Jacky Charbo Nneau.
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko, Nassor Ahmed Mazrui (kushoto), akibadilishana Nyaraka za Utiaji Saini Mkataba wa Uwekaji wa Nembo ya Karafuu ambayo itatumika katika Zao la Karafuu ya Zanzibar na Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Kulinda Haki za Ubunifu (WIPO), Neema Nyerere, katika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar.
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui (kushoto), akipeana Mikono na Mkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha Biashara (ITC), Jacky Charbo Nneau, baada ya Utiaji saini Mkataba wa Uwekaji wa Nembo ya Karafuu ambayo itatumika katika Zao la Karafuu ya Zanzibar hapo katika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar jana.
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko, Nassor Ahmed Mazrui (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Kulinda Haki za Ubunifu (WIPO), Neema Nyerere (kushoto yake) na Mkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha Biashara (ITC), Jacky Charbo Nneau (kulia kwake) pamoja na wajumbe mbalimbali waliohudhuria katika hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Uwekaji wa Nembo ya Karafuu, ambayo itatumika katika Zao la Karafuu ya Zanzibar katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Grand Palace, Malindi Mjini Zanzibar jana. (Picha zote na Yussuf Simai - Maelezo Zanzibar)
No comments:
Post a Comment