TANGAZO


Sunday, November 18, 2012

TEA yakusanya mil. 50 Dar es Salaam katika matembezo ya hisani kuchangia ujenzi mabweni ya wanafunzi wa kike wa Sekondari



 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu (katikati), akiongoza matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wanafuzi wa kike. Kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Rosemary Lulabuka na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Dk. Naomi Katunzi. 
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Makongo wakishiriki katika matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa mambweni ya wasichana, yaliyoanzania Mlimani City na kuishia katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo. Jumla ya sh. milioni 50  ikiwa ni pamoja na ahadi zilipatikana.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani, wakiwa katika matembezi hayo ya hisani ya kuchangia ujenzi wa mambweni ya wasichana, yaliyoanzania Mlimani City na kuishia katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo. 
Askari Polisi na mmoja wa washiriki wa Matembezi hayo, wakionesha furaha yao wakati wakitembea.
Baadhi ya wadau walioshiriki matembezi hayo, wakiwa wamejipumzisha baada ya matembezi hayo.
Baadhi ya wanafunzi wasichana wa Shule za Sekondari jijini Dar es Salaam wakiwa wamejipumzisha baada ya kumalizika matembezi hayo.
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Rosemary Lulabuka akizungumza mara baada ya kumalizika kwa matembezi hayo.
 Balozi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wasichana, akizungumza mara baada ya kumalizika matembezi.
Balozi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wasichana, Faraja Nyalandu, akizungumza baada ya kumalizika matembezi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu akizungumza mara baada ya kumalizika matembezi hayo.
 Naibu Waziri wa Maliasilia na Utalii, Lazaro Nyarandu akiwa na mkewe, ambaye pia ni balozi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wasichani, Faraja Nyalandu, ambapo alichangia sh. milioni 10 kwa ajili ya kusadia ujenzi wa mabweni ya wasichana. 
 Naibu Waziri wa Maliasilia na Utalii, Lazaro Nyarandu akipeana mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Dk. Naomi Katunzi baada ya kuchangia sh. milioni 10 kwenye matembezi hayo.
 Michango ikiendelea kukusanywa kwa njia ya mitandao.
 Wadau wakiselebuka wakati wa kumalizika matembezi hayo.
Msanii Barnabas Elius, akitumbuiza wakati wa hafla ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Baobab (katikati), akiimba pamoja na wanamuziki wa bendi ya THT, wakati wa matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa kike, yaliyoanzia Mlimani City na kumalizikia katika viwanja vya Chuo Kikuu (UDSM), jijini Dar es Salaam leo.
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Baobab, Khadija Nuru akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake ambao walichangia kiasi cha sh. milioni 1. (Picha zote kwa hisani ya Habari Mseto Blog)

No comments:

Post a Comment