TANGAZO


Monday, November 5, 2012

Omani kujenga kituo kikubwa cha elimu ya Dini ya Kiislamu Zanziar

Balozi Mdogo wa Oman nchini, Sheikh Mansoor, akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika moja ya mikutano yake mjini Zanzibar.

Na Ali Issa Maelezo Zanzibar
5/11/2012
SERIKALI  ya Omani inakusudia kujenga kituo cha elimu ya dini ya Kiislamu Zanziar  kitakacho beba mitaala  ya elimu ya dini hiyo ili kuifanya Zanzíbar kuwa bora Kitaifa na Kimatifa katika kusimamia mitaala mizima ya dini ya Kiislamu .


Hayo yamesemwa leo huko Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali  mjini Zanzibar na Balozi mdogo wa Omani aliyepo Zanzibar, Mansoor Nasser Mansoor wakati wa mazungumzao kati yake na Jopo la Mainjinia kutoka Kampuni mbalimbali wa ndani na nje ya nchi ambao wanawania  tenda ya ujenzi wa kituo hicho.

Amesema ujenzi wa kituo hicho ni pamoja  na ujenzi wa msikiti utakao kuwa na uwezo wa kuswaliwa na waumini 3500 kwa wakati mmoja. Pia alisema kuwa utakwa na madrasa, kumbi za mikutano maktaba za kisasa,maabara   na mambo mengine yanayo usiana na maadili ya kiislamu.

"Ni kuwapendelea  Waislamu wa Zanzíbar, kwani hii ni fursa yao na waitumie  ili waweze kunufaika na ujenzi huu na waitumie vizuri kwani ni faida kwao na  vizazi vijavyo katika masuala mazima ya dini ya Kiislamu ". Alisema Balozi Mansoor.

Aidha, Balozi huyo alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho ni muendelezo wa misaada yao kwa Zanzibar kwani Zanzibar na Omani ni marafiki wa muda mrefu na watu wake wana  uhusiano wadamu.

Amesema chuo hicho,  kitaifanya  Zanzíbar kuwa na fursa kubwa ya  kuendelea kuwa kitovu cha dini  ya Kiislamu kwa vile asilimia kubwa ya wananchi wake  ni waislamu.

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Abdalla Mzee alisema kuwa, ujenzi wa kituo hicho ni utanuzi wa Chuo  cha Kiislam kilichopo mjini humo na kuweza kukifanya chuo hicho, kuwa Chuo Kikuu cha Kiislamu Zanzibar.

Alisema ujenziwa kituo hicho utakuwa na urefu wa mita 14000 na mita 4000 za mraba ambapo zabuni yake itaisha tarehe 17, Disemba mwaka huu .

Naye Mkuu wa Chuo cha Kiislamu, Mwalimu Siasa, alisema kuwa hali hiyo
ni yakufurahisha kwa Wazanzibar kwani hiyo ndio njia moja wapo ya utanuzi wa elimu ya Dini ya Kiislamu na kuwafanya waumini wa dini hiyo, kuwa na upeo zaidi wa ufahamu wa  dini yao.

Alisema  chuo kiliopo kina  changa moto nyingi ikiwemo ukosefu wa miundo mbinu, Hivyo kituo hicho kitakua ni chachu ya kujipatia taaluma na misingi bora ya Dini na kuondoa ufinyu uliopo kwa baadhi ya mambo ya kitaaluma .

No comments:

Post a Comment