TANGAZO


Saturday, November 24, 2012

Dk.Salim Ahmed Salim awa mgeni rasmi Mahafali ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, waandishi watawala

Baadhi ya wahitimu wa shahada mbalimbali wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA) , wakiwa kwenye mahafali yao chuoni hapo leo, ambapo Waziri Mkuu  mstaafu, Salim Ahmed Salim, alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, Kigamboni, Dar es Salaam.Kulia ni mmoja wa waandishi wa habari aliyehitimu mahafali hayo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), wakitunukiwa shahada zao na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, Kigamboni, Dar es Salaam leo.

Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), wakifuatilia matukio ya kutunukiwa shahada na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, Kigamboni, Dar es Salaam leo. Kulia ni mwandishi wa habari, Saphia Ngalapi.

Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), wakiwa na nyuso za furaha wakati wa mahafali hayo, ambayo wahitimu walitunukiwa shahada mbalimbali na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, Kigamboni, Dar es Salaam leo. Kulia ni mmoja wa waandishi wa habari, waliotunukiwa shahada katika mahafali hayo.

Mwandishi wa habari wa magazeti ya Mwananchi, George Njogopa, akiwa katika mahafali hayo, wakati alipokuwa akitunukiwa Shahada ya Siasa na Maendeleo ya Jamii na mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya chuo hicho, Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim.

Mwandishi wa habari, Furaha Tonya wa ITV (katikati), akiwa na baadhi ya wahitimu wenzake, Witness Tenende (kushoto) na Tido Joseph (kuli), wakiwa wamesimama wakati walipokuwa wakitunukiwa shahada zao katika mahafali hayo leo, chuoni hapo.

Mwandishi wa habari, Furaha Tonya wa ITV (kulia) na rafiki yake, Witness Tenende, wakifurahi baada ya kutunukiwa shahada zao katika mahafali hayo leo, chuoni hapo.

Mwandishi wa habari, Furaha Tonya wa ITV (kulia) na rafiki yake, Witness Tenende (kushoto), mtoto wake, Charity Ntine pamoja na mama na mdogo wake wakipiga picha ya kumbukumbu mara baada ya kutunukiwa shahada zao katika mahafali hayo leo, chuoni hapo.

Wahitimu wakibadilishana mawazo kwenye mahafali yao hayo.

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, akitunuku shahada kwenye mahafali hayo, chuoni hapo leo. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Dk. John Magoti.

Wahitimu wakifurahia mahafali yao.

Wahitimu wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka katika mahafali yao hayo.

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, akiondoka baada ya kuyafunga mahafali hayo, chuoni hapo leo. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Dk. John Magoti.

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kuyafunga mahafali hayo yaliyofanyika chuoni hapo leo. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Dk. John Magoti.

Mwandishi wa habari, Saphia Ngalapi (kulia), akipiga picha ya kumbukumbu pamoja na familia yake, mara baada ya kutunukiwa shahada katika mahafali hayo.

Mwandishi wa habari wa magazeti ya Mwananchi, George Njogopa (kulia), akiwa pamoja na mmoja wa walimu wake, mhadhiri na Afisa Ubora wa Chuo, Parit Ole Saruni (katikati) na mhitimu mwenzake Mohamed Soud Bakari, wakipiga picha ya kumbukumbu ya mahafali hayo.

Mwandishi wa habari, Saphia Ngalapi (katikati), akipewa shada la maua na mmoja wa wanafamilia yake, mara baada ya kutunukiwa shahada katika mahafali hayo.
.
Mwandishi wa habari, Saphia Ngalapi (katikati), akipiga picha ya kumbukumbu na familia ya jamaa yake huyo, ili kupata kumbukumbu ya tukio hilo.

Mwandishi wa habari, Saphia Ngalapi, akifurahia ua lake hilo, alilokabidhiwa na jamaa yake huyo.

Mwandishi wa habari, Saphia Ngalapi (wa pili kushoto), akifurahia jambo pamoja na baadhi ya wahitimu wenzake wakati walipokuwa wakibadilishana mawazo kwenye mahafali yao hayo.

No comments:

Post a Comment