Afisa Misitu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Freddy Manyika akitoa nasaha zake kwa kusema kuwa sisi wananchi ndio tunatakiwa kuwa wa kwanza kufanya mabadiliko na sio kuilaumu serikali kwani ndio tunaozungukwa na mazingira. Aidha pia ametumia nafasi hiyo kutangaza kuwa suala la mabadiliko ya hali ya hewa sio jambo la mzaha, hivyo kuitaka Serikali kuwa na sera madhubuti zitakazo wawezesha wananchi kukabiliana na madhara yatokanayo na janga hilo, ili kujitahidi kuirejesha ardhi na mazingira yetu kwa ujumla katika hali bora.
Mtaalamu wa Ikolojia, Profesa Raphael Mwaliosi akitoa mada wakati wa majadiliano ya hadhara, yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN), ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja huo, ambapo amechambua changamoto baina ya Mazingira na Mabadiliko ya hali ya hewa hapa nchini na jitihada za kukabiliana nazo. Ameongeza kuwa changamoto zaidi zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa zinaleta athari mpaka katika nyanja za kiuchumi, akitolea mfano sekta za Kilimo, Maji, Nishati, Afya, Misitu, Uvuvi na Utalii.
Mmoja wa wanafunzi kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali jijini Dar es Salaam, akitoa maoni yake katika mjadala wa wazi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee, ambapo wamelalamikia baadhi ya Sera za Serikali zisizotekelezeka, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa kusheherekea miaka 67 ya umoja huo .
Baadhi ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu mbalimbali jijini Dar es Salaam waliohudhuria mjadala huo wa wazi ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN), wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa katika kusheherekea miaka 67 tangu kuanzishwa kwake.
Baadhi ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu mbalimbali jijini Dar es Salaam waliohudhuria mjadala huo wa wazi ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN), wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa katika kusheherekea miaka 67 tangu kuanzishwa kwake. (Picha zote na John Bukuku wa Fullshangwe)

No comments:
Post a Comment