Msanii wa bongo fleva, Ommy Dimpoz akitumbuiza na densa wake jukwaani kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ambalo limemalizika usiku wa kuamkia leo na kukusanya mashabiki kibao kutoka pande mbalimbali za jiji la Mwanza. Tamasha hilo la Serengeti Fiesta 2012, limefanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba. Katika tamasha hilo mshindi aliyejishindia gari aina ya Vits ambazo zimekuwa zikitolewa na kampuni ya Push Mobile katika mchakato mzima wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ni Bahati Joseph, mkazi wa jiji la Mwanza na ni mjasiriamali.
Msanii Mwasiti Almasi, akifanya vitu vyake jukwaani katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012, lililofanyika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Push Mobile, Rugambo Rodney (kushoto), akimkabidhi fungua ya gari Bahati Joseph, ambaye ameibuka mshindi wa gari aina ya Vitz.
Umati wa mashabiki waliohudhuria katika tamasha hilo, ukifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitokea kwenye tamasha hilo.
Wasanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu (kulia) na Aunt Ezekiel wakifanya vitu vyao jukwaani katika tamasha hilo.
Msanii wa Vichekesho Steve Nyerere, akimuangalia msanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu wakati alipokuwa akiimba moja ya wimbo wa mwanamziki aliyekuwa mpenzi wake, Diamond.
Msanii wa Bongo Movie, Raymond Kigosi 'Ray' (kushoto) na Wema Sepetu, wakiimba pamoja jukwaani.
Msanii wa maigizo, Wema Sepetu, akiimba huku wenzake wakifurahia jukwaani. Kushoto ni Raymond Kigosi na kulia ni Aunt Ezekiel, Steve Nyerere na Steven Jacob 'JB'.
Kutoka kulia ni Steve Nyerere, Dj Fetty wa Clouds, Raymond Kigosi, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wakichuana kusakata muziki.
Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akisoma namba ya mshindi aliyejishindia gari aina ya Vitz, ambazo zimekuwa zikitolewa na Kampuni ya Push Mobile katika mchakato mzima wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012. Katikati ni Meneja Masoko wa kampuni ya Push Mobile, Rugambo Rodney na kushoto ni mmoja wa wakilishi wa Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha, Abubakari Maggid, wakishuhudia tukio hilo, usiku wa kuamkia leo, ndani ya uwanja wa CCM Kirumba. Mshindi wa gari hilo aina ya Vitz, alitajwa kuwa ni Bahati Joseph, mkazi wa jiji la Mwanza, ambaye ni mjasiriamali.
![]() |
| Umati wa mashabiki ukishuhudia matukio yaliyokuwa yakitendeka uwanjani hapo, usiku wa kuamkia leo jijini Mwanza. |
Msanii Recho kutoka THT, akiwa sambamba na densa wake wakionesha umahiri wa kuimba na kuzirudi ngoma jukwaani.
![]() |
| Baadhi ya wadau wakipozi kwa picha wakati wa tamasha hilo. |
![]() |
Msanii Recho kutoka THT, akiimba moja ya nyimbo zake kwenye tamasha hilo, uwanjani hapo. |
Sehemu ya umati wa watu ukishangilia vilivyo, matukio yaliyokuwa yakitendeka usiku wa kuamkia leo, ndani ya uwanja wa ccm Kirumba, jijini Mwanza.
Msanii Ney wa Mitego kama kawa akikamua kwa hisia, mbele ya wakazi wa jiji la Mwanza (hawapo pichani), waliojitokeza kwa wingi ndani ya uwanja wa CCM Kirumba kushuhudia tamasha hilo.
![]() |
| Mmoja wa wasanii waliotumbuiza kwenye tamasha hilo, akiimba huku wacheza shoo wake wakionesha ufundi wa kuzirudi ngoma kwenye tamasha hilo. |
Msanii machachari katika muziki wa kizazi kipya, Mwasiti Almasi akiimba jukwaani katika tamasha hilo.
![]() |
| Mmoja wa wasanii waliokuwa wakitumbuiza kwenye tamasha hilo, akifanya vitu vyake mbele ya umati wa watazamaji uwanjani hapo. |
Masharobaro kazini, Bob Junior na kundi lake wakitumbuiza kwenye tamasha hilo, uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya aka Bongo fleva, Profesa Jay, akishusha mistari yake kama kawa mbele ya umati wa watu waliojitokeza (hawapo pichani), usiku wa kuamkia leo, ndani ya uwanja wa CCM Kirumba.
Mashabiki waliofurika kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, lililofanyika uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza, wakiripuka kwa furaha baada ya kuridhishwa na burudani iliyokuwa ikitolewa kwenye tamasha hilo, viwanjani hapo usiku wa kuamkia leo, jijini Mwanza. Wasanii mbalimbali wa muziki wa Bongo Fleva wamepanda jukwaani wakiwemo wale wa Bongo Movie, wakiongozwa na akina JB, Steven Nyerere, Aunt Ezekiel, Wema Sepetu, Vicent Kigosi 'Ray' na wengine wengi kama inavyoonekana katika matukio pichani.
| Umati wa mashabiki ukifuatilia matukio hayo uwanjani hapo usiku wa kuamkia leo, jijini Mwanza. |
| Mashabiki ilikuwa ni mbele kwa mbele tu hapana kurudi nyuma, kila mmoja akitaka apate kuwaona kwa karibu wasanii waliokuwa wakitumbuiza kwenye tamasha hilo, uwanjani hapo. (Picha zote na John Bukuku wa Fullshangwe.blogspot) |













No comments:
Post a Comment