TANGAZO


Wednesday, September 5, 2012

Wanahabari Iringa wagoma kupokea ripoti ya Awali ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, kufatia kifo cha Daudi Mwangosi


DCI Robert Manumba

                                                    Baadhi ya wanahabari 
                      Wanahabari wa Iringa Wakitoka nje ya ofisi
Wanahabari wa Iringa mchana wa leo wamegoma kupokea taarifa ya awali ya uchunguzi wa kifo cha Mwandishi Daudi Mwangosi, aliyeuawa juzi jumapili katika mkutano wa ndani wa Chadema uliokuwa ufanyike katika kijiji cha Nyololo Iringa. Mkuu huyo alikataa shariti la wandishi la kumtaka atoe taarifa hiyo bila kuwepo kwa Polisi yeyote katika mkutano huo. Kitendo hicho cha mkuu huyo kukataa shariti  la wanahabari kikapelekea waandishi kutoka nje ya ukumbi huo.cHivyo zoezi hilo kushindikana. (Picha na habari , Said Ng'amilo, Mjengwablog-Iringa)

No comments:

Post a Comment