TANGAZO


Monday, September 3, 2012

Viongozi wa nchi wajumbe wa asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (TROIKA) ya Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC), kukutana Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika) ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), akimpokea Rais Armando Guebuza wa Msumbiji baada ya kuwasili leo Septemba 3, 2012 katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Slaam, tayari kwa mkutano wa Troika ya SADC unaotarajiwa kufanyika kesho Septemba 4, 2012 Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency na kuhudhuriwa na viongozi wa nchi wajumbe wa Asasi hiyo ambao ni Msumbiji ambao ni Mwenyekiti wa sasa wa SADC, Afrika Kusini aliyekuwa Mwenyekiti wa Asasi hiyo kabla ya Tanzania, Namibia ambao ni Makamu Mwenyekiti wa Asasi hiyo ya Troika, pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambao ni wageni waalikwa.(Picha na Ikulu)

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika) ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), akiongozana na  Rais Armando Guebuza wa Msumbiji wakati alipokagua gwaride la Heshima lililoandaliwa kwa ajili yake kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere., Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika) ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)  Rais Armando Guebuza wa Msumbiji wakiondoka kwenye uwanja wa ndege wa Mawlimu J.K.Nyerere leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete,  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika) ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), akimuonesha Rais Armando Guebuza wa Msumbiji mandhari ya Bandari ya Dar es Salaam kutoka  katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency,  baada ya kuwasili leo Septemba 3, 2012 tayari kwa mkutano wa Troika ya SADC unaotarajiwa kufanyika kesho Septemba 4, 2012 hotelini hapo na kuhudhuriwa na viongozi wa nchi wajumbe wa Asasi hiyo ambao ni Msumbiji ambao ni Mwenyekiti wa sasa wa SADC, Afrika Kusini aliyekuwa Mwenyekiti wa Asasi hiyo kabla ya Tanzania,  Namibia ambao ni Makamu Mwenyekiti wa Asasi hiyo ya Troika, pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambao ni wageni waalikwa. (Picha na Mdau wetu)

No comments:

Post a Comment