Msanii chipukizi wa muziki wa Hip Hop, kutoka Serengeti Super Nyota, Young Killer, akiwajibika jukwaani, katika tamasha la Serengeti Fiesta, 2012, lililofanyika Uwanja wa Mwalimu Nyerere, usiku wa kuamkia leo, mjini Shinyanga.
Mashabiki wakifuatilia kwa ukaribu tamasha la Serengeti Fiesta, Shinyanga usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Kambarage.
Mmoja wa wasanii wakike, wanaochipukia, akiburudisha uwanjani hapo.
Mwimbaji wa muziki wa mduara, IT akionesha manjonjo yake katika tamasha la Serengeti Fiesta, lililofanyika mkoani Shinyanga usiku wa kuamkia leo.
Mashabiki wakifurahia burudani iliyokuwa ikitolewa katika tamasha la Serengeti Fiesta, mkoani Shinyanga.
Profesa Jay, akifanya vitu vyake katika Uwanja wa Kambarage, mkoani Shinyanga, wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Msanii Ommy Dimpozi, akicheza na shabiki wake.
Msanii Ney wa Mitego, akikamua katika tamasha la Serengeti Fiesta.
Msanii Barnabas akijibu mapigo kwa shabiki wake, kwenye tamasha la Serengeti Fiesta, lililofanyika usiku wa kuamkia leo, mkoani Shinyanga.
Mh.Temba, akiwapa mikono mashabiki wake katika tamasha la Serengeti Fiesta.
Mtangazaji wa Clouds TV, Antonio Nugaz, akitangaza washindi wawili wa pikipiki zinazotolewa na kampuni ya Push Mobile.
Msanii wa muziki wa Hip Hop, Roma akifanya vitu vyake uwanjani hapo katika tamasha la Serengeti Fiesta.
Waimbaji wa kundi la Wanaume Family, Mh. Temba, Chege na Bibi Cheka wakifanya vitu vyao katika tamasha la Serengeti Fiesta.
Msanii Ommy Dimpozi, akiimba mbele ya mashabiki wake.
Mashabiki wakifurahia burudani za Serengeti Fiesta, mkoaani Shinyanga.
Mashabki wakipata burudani za Serengeti Fiesta, mkoani Shinyanga usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Kambarage. (Picha na mdau wetu)

















No comments:
Post a Comment