Mtafiti kutoka China Miao Zhong, akimuonesha Naibu Waziri Mkuu wa China, Hui Liangyu (kulia kwa aliyepeleka mkono kwenye uso), njia ya Reli ilipoanzia kwa upande wa Tanzania. Naibu Waziri Mkuu wa China alikuwa na ziara katika Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) leo asubuhi.
Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe, akimkaribisha Naibu Waziri Mkuu wa China Hui Liangyu, katika Stesheni ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA). Naibu Waziri Mkuu wa China alikuwa na ziara ya kuangalia namna Stesheni hiyo, inavyofanya kazi. Serikali ya China imetuma wataalamu kwa ajili ya kufanya utafiti wa namna ya kuiboresha Mamlaka hiyo.

No comments:
Post a Comment