Pages

Thursday, August 9, 2012

Wabunge wa CCM Zanzibar waunga mkono Muungano wa Serikali mbili

Mbunge wa Uzini Muhammed Seif Khatib
Na Joyce Kassiki,Dodoma

PAMOJA na wananchi wengi wakiwemo viongozi wa ngazi za juu Visiwani Zanzibar kukataa muungano wa Serikali mbili, lakini wabunge wa CCM kutoka Zanzibar wameibuka na kutoa tamko lao la kuunga mkono muungano huo.
 Akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari mjini hapa mara baada ya kuahirishwa kwa kikao cha Bunge saa saba mchana leo, Mwenyekiti wa wabunge hao ambaye pia ni Mbunge wa Uzini  Muhammed Seif Khatib (CCM)alisema , wanaungana mkono muundo na mfumo huo kwani waamini baada ya mabadiliko  kadhaa kwa vipengele vy a katiba vitapelekea kutoa haki kwa nchi mbilihizo  zilizofanya muungano huo.
Alisema muundo huo wa  Serikali mbili, utaondoa kero baada ya kufanyika marekebisho ya kero za msingi za Muungano na hatimaye mfumo huo kuwa na tija kwa wananchi wake.
“Katika muundo wa mfumo huo wa Muungano,sisi wabunge wa CCM kutoka Zanzibar,tunaunga mkono muundo na mfumo wa Serikali mbili pamoja na mabadiliko kadhaa kwa vipengele vya katiba ambavyo hatimaye vitapelekea kutoa haki kwa nchi zetu mbili zilizofanya muungano huu,
 “Katika Ilani ya Uchaguzi tuliyoitumia ss wabunge wa CCM kuomba ridhaa kwa wananchi na kushinda,inasisitiza juu muundo wa Serikali mbili inayosema’kuendeleza muundo wa Serikai mbili zilizopo sasa na kudumisha ushirikiano mwema kati ya Serikali hizi’,
 “Hivyo kwa kuizngatia maamuzi ya chama na maelekezo ya Ilani ya uchaguzi,ssi wabunge wa CCM kutoka Zanizbar kwa kauli moja tunaunga mkono muundo wa muungano wa Serikali mbili,Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Muungano wa Tanzania.”aisema
 Pia alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wapiga kura wa Zanzibar na wazanzibar wote kwa ujumla waendelee kkuwaunga mkono katika msimamo huo wa Serikali mbili.
Vile vile aliwataka wananchi hao kujikita katika maeneo mbalimbali katika kutoa maoni yao kwenye mchakto wa katiba mpya na siyo kujikita katika eneo moja tu la Muungano.
Alisema yapo maeneo mengi ambayo wakiyazungumza kwenye mchakato huo yatakuwa na manufaa kwao na Taifa kwa ujumla.




No comments:

Post a Comment