TANGAZO


Saturday, August 11, 2012

Mitt Romney ateua mwenza

Mgombea urais wa Marekani kwa niaba ya chama cha Republican, Mitt Romney, amtangaza makamu wake.
Paul Ryan (kushoto) na Mitt Romney
Duru kwenye kampeni za uchaguzi aliviambia vyombo vya habari vya Marekani, kwamba Bwana Romney amemteua Paul Ryan, mwenye umri wa miaka 42, na mwenyekiti wa kamati ya bajeti ya bunge.
Bwana Ryan ameahidi kubatilisha mageuzi yaliyofanywa na Rais Obama katika huduma ya afya, na anapendelea matumizi ya serikali yapunguzwe sana.
Mwandishi wa BBC anasema chaguo la Paul Ryan litazidisha kuleta tofauti kuhusu jinsi uchumi wa Marekani unavofaa kushughulikiwa.

No comments:

Post a Comment