Wananchi wakisubiri kuingia ndani ya ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa nane, katika kikao cha 46 cha Bunge ambapo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliwasilisha hotuba ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2012/2013.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu uamuzi wa Serikali wa kuwafukuza kazi watumishi watatu wa Wizara hiyo kutokana na ukiukaji wa Sheria na utekelezaji wa majukumu yao ya kazi kufuatia sakata la usafirishaji wa wanyama pori kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwenda Quatar.
Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (kulia), akiongea jambo na Mbunge wa Dole, Sylvester Mabumba, nje ya ukumbi wa Bunge leo, mjini Dodoma. Dk. Kawambwa amewasilisha hotuba ya Wizara hiyo leo, ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2012/2013.
Baadhi ya wadau wa Elimu, wakifuatilia kwa makini hotuba ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2012/2013, iliyokuwa ikisomwa leo, mjini Dodoma Waziri wa wizara hiyo, Dk. Shukuru Kawambwa.
Baadhi ya wadau wa Elimu akifuatilia kwa makini hotuba ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya mapato na matumizi, iliyokuwa ikisomwa na Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Shukuru Kawambwa.
No comments:
Post a Comment