TANGAZO


Monday, August 6, 2012

CAG kukagua Hesabu za Umoja wa Mataifa

Edwin Rweyemamu kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), akimkaribisha CAG, ambaye pia ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Umoja wa Mataifa (UN), Ludovick Utouh ili aweze kuongea na waandishi wa habari, kuhusu Tanzania kupata nafasi ya kukagua hesabu za UN kwa kipindi cha miaka sita. Watumishi 60 kutoka Ofisi ya CAG, watafanya kazi ya kuzikagua taasisi 10 za UN. 

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambaye pia ni Mkaguzi wa Hesabu za Umoja wa Mataifa  (UN), Ludovick Utouh akiongea na waandishi wa habari kuhusu Taasisi 10 za UN, ambazo zitafanyiwa ukaguzi chini ya usimamizi wake ambapo watumishi 60, kutoka ofisini kwake watafanya kazi hiyo. Kwa kipindi cha miaka sita nchi za Tanzania, China na Uingereza zimepewa jukumu la ukaguzi  wa hesabu za UN.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) ambaye pia ni Mkaguzi wa hesabu za Umoja wa Mataifa  (UN) Ludovick Utouh akielezea jambo kwa waandishi wa habari , Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akizungumza nao, kuhusu  Taasisi 10 za UN ambazo zitafanyiwa ukaguzi chini ya usimamizi wake ambapo watumishi 60 kutoka ofisini kwake watafanya kazi hiyo. 

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG), ambaye pia ni Mkaguzi wa Hesabu za Umoja wa Mataifa  (UN), Ludovick Utouh akifafanua jambo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu  Taasisi 10 za UN, ambazo zitafanyiwa ukaguzi chini ya usimamizi wake ambapo watumishi 60 kutoka ofisini kwake watafanya kazi hiyo. 


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG), ambaye pia ni Mkaguzi wa hesabu za Umoja wa Mataifa (UN), Ludovick Utouh akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu Taasisi 10 za UN ambazo zitafanyiwa ukaguzi chini ya usimamizi wake. (Picha zote na Anna Nkinda – Maelezo)

No comments:

Post a Comment