TANGAZO


Thursday, August 9, 2012

Balozi Mahalu ashinda kesi ya kuhujumu Uchumi


 Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu akikumbatiana kwa furaha na mdogo wake Mirasi Rama baada Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, kumuachia huru katika kesi ya kuhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabili. 


 Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, akikumbatiana kwa furaha na mmoja wa ndugu zake baada ya kushinda kesi yake katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam leo, wakati wa kutolewa hukumu wa kesi yake ya kuhujumu uchumi na kuisababishia hasara Serikali ya Euro milioni 2, wakati akiwa balozi nchini humo. Profesa Mahalu ameshinda katika hukumu iliyotolewa na Mahakama hiyo.

Mahalu akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuachiwa huru na Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam leo. 
 Profesa Costa Mahalu (katikati), akitoka nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam huku akiongozana na wakili wake, Mabere Nyaucho Marando , aliyeshika mafaili kushoto.
  Profesa Costa Mahalu, akipeana mkono na mmoja wa ndugu waliofika mahakamani hapo wakati wa hukumu hiyo.
 Profesa Costa Mahalu akizungumza na mwaandishi wa Deuch Welle, Abubakar Liongo, nje ya Mahakama hiyo leo mchana.


 Mmoja wa washitakiwa aliyeshitakiwa pamoja na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, Grace Martine (katikati), akisaidiwa na ndugu zake kutoka Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam leo, baada ya kushinda kesi yao ya kuhujumu uchumi na kuisababishia hasara Serikali ya jumla ya Euro milioni 2.

 Aliyekuwa Ofisa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, ambaye alishitakiwa pamoja na Profesa Mahalu katika kesi hiyo, Grace Martin (katikati), akisaidiwa na ndugu zake, akitoka Mahakamani, huku akihojiwa na mwaandishi wa Deuch Welle, Abubakar Liongo, baada ya hukumu hiyo, iliyowaachia huru. 

Grace Martin (katikati), akiwa na ndugu zake, nje ya Mahakama ya Kisutu baada ya  hukumu hiyo, iliyowaachia huru. 

Wakili wa kesi ya Mahalu,  Mabere Marando, akizungumza na vyombo vya habari baada ya hukumu hiyo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

No comments:

Post a Comment