Wachezaji wa Mtibwa wakiswali kushukuru na kushangilia goli la kwanza la timu hiyo dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Chamazi, jijini Dar es Salaam. Mtibwa ilishinda mabao 2-0 katika mchezo huo wa Ligi ya Super 8, inayodhaminiwa na BacABC.
Wachezaji wa Mtibwa wakipongezana baada ya Shaaban Kisiga kuipatia timu hiyo goli la kwanza dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Chamazi, jijini Dar es Salaam, katika mchezo huo wa Ligi ya Super 8, inayodhaminiwa na BacABC.
Said Morad wa Azam FC, akilala chini kuuondoa mpira miguuni mwa Jamal Mnyate wa Mtibwa Sugar katika mchezo huo.
Mshambuliaji wa Azam FC, akijaribu kumpiga chenga Babuu Ally Seif wa Mtibwa.
Mchezaji wa Azam FC, akilala chini kuuondoa mpira miguuni mwa mshambuliaji wa Mtibwa Sugar.
Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Shaaban Kisiga (kulia), akimtoka golikipa wa Azam FC (aliyelala chini), baada ya kumpiga chenga na kufunga moja ya magoli ya timu hiyo.
Mchezaji Jamal Mnyate wa Mtibwa akitafuta mbinu ya kumpita Abdulhalim Humud wa Azam FC, wakati wa mchezo huo wa Sper 8, uliochezwa Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam leo jioni ambapo Mtibwa ilishinda mabao 2-0.
Mashabiki wachache waliohudhuria kuangalia mchezo huo, wakifuatilia kwa makini matukio ya uwanjani kati ya wachezaji wa timu hizo walipokuwa wakipambana kuusaka ushindi.










No comments:
Post a Comment