Mkuu wa kundi la Kiislam ambalo limechukua udhibiti wa kaskazini mwa Mali anasema amepokea juhudi za upatanishi za Burkina Faso.
Kiongozi wa Ansar Dine, Iyad Ag Ghaly alikuwa akizungumza baada ya kukutana na Waziri wa Mambo nje wa Burkina Faso Djibril Bassole katika mji wa kaskazini wa Kidal.
Bw Bassole ni mwanadiplomasia mwandamizi kutembelea eneo hilo lilochukuwa na vikosi vya Kiislam vya Tuareg mwezi Machi.
Viongozi wa Afrika Magharibi wamesema watatuma vikosi vya majeshi yapatao 3000 kuingilia kati mzozo wa Mali.
Hata hivyo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa bado halijapitisha hoja hiyo, kwa kuogopa kwamba kuivamia kijeshi nchi hiyo inaweza kugharimu na kuchukua muda mrefu.
Vikosi vya waasi wa kaskazini mwa Mali waliteka eneo hilo baada ya jeshi kufanya mapinduzi mwezi Machi.
Kundi hilo la kiislam linadhibiti miji mitatu mikubwa ya Gao, Timbuktu na Kidal - baada ya kuangukia mikononi mwa makundi ya Tuareg ambayo yamekuwa wakipigania uhuru wa eneo hilo.
Makundi hayo ya kiislam yamekuwa yakishutumiwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu kwa ajili ya kuharibu makaburi ya kale katika mji wa Timbuktu na kuwaadhibu kwa kuwapiga mawe hadi kufa watu wasiokuwa na ndoa ambao walidaiwa kufanya mapenzi nje ya ndoa wiki iliyopita.
No comments:
Post a Comment