Mgeni rasmi katika ufunguzi wa tsn Super Market Tegeta, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, akilakiwa na uongozi wa Makampuni ya tsn, wakati alipowasili kwenye jengo la Kibo Plaza kwa ajili ya kuzindua tsn Super market Tegeta jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Makampuni hayo, Forough Baghozah na wa kwanza ni Naibu Meya wa Kinondoni, Songoro Mnyonge. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa tsn Super Market Tegeta, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, akisindikizwa na uongozi wa Makampuni ya tsn, kuelekea kwenye ukumbi wa mkutano mara baada ya kuwasili kwenye jengo la Kibo Plaza kwa ajili ya kuzindua tsn Super market, Tegeta jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Makampuni hayo, Forough Baghozah, Mkrugenzi wa tsn, Emmanuel Ngallah (kushoto) na Mkurugenzi wa tsn Oil, Ahmed Baghozah.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa tsn Super Market Tegeta, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, akiwa na Mwenyekiti wa Makampuni hayo, Forough Baghozah (kulia) na Naibu Meya wa Kinondoni, Songoro Mnyonge, wakati wa hafla hiyo leo asubuhi.
Baadhi ya wageni na wananchi waliofika kwenye uzinduzi huo, wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka kwenye ukumbini hapo.
Mkurugenzi wa tsn Super Market Ltd, Fahad Baghozah, akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu wakati wa uzinduzi wa tsn Super market, Tegeta jijini leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Mary Nagu, akitoa hotuba yake, wakati alipokuwa akizundua Super market hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Makampuni hayo, Forough Baghozah na kushoto ni Naibu Meya wa Kinondoni, Songoro Mnyonge.
Baadhi ya wafanyakazi wa Super market ya Tegeta, wakifurahia uzinduzi huo, uliofanywa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Mary Nagu, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa tsn Super market hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Makampuni hayo, Forough Baghozah na kushoto ni Naibu Meya wa Kinondoni, Songoro Mnyonge.
Mkurugenzi wa tsn Super Market Ltd, Fahad Baghozah, akifungua shampeni, wakati wa uzinduzi huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, akigonganisha glasi yenye shampeni na Naibu Meya wa Kinondoni, Songoro Mnyonge (katikati) na Mkurugenzi wa tsn, Emmanuel Ngallah (kushoto), wakati alipozindua tsn Super market hiyo jijini leo.
Viongozi wa Makampuni ya tsn, wakigonganisha glasi kwa ajili ya kutakiana heri katika uzinduzi wa tsn Super market, Tegeta jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Makampuni hayo, Forough Baghozah.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa tsn Super Market Tegeta, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, akinyanyua juu glasi ya shampeni pamoja na uongozi wa Makampuni ya tsn, wakati alipozindua tsn Super market kwenye jengo la Kibo Plaza Tegeta, jijini Dar es Salaam leo. Wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa Makampuni hayo, Forough Baghozah.
Mwenyekiti wa Makampuni ya tsn, Forough Baghozah, akizungumza na waandishi wa habari ndani ya tsn Super market ya Tegeta, mara baada ya kuzinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu leo asubuhi.
Baadhi ya wananchi wakiwa ndani ya tsn Super market, mara baada ya kuzinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, Tegeta jijini leo.
Baadhi ya wananchi wakichagua bidhaa za kununua ndani ya tsn Super market, mara baada ya kuzinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, Tegeta jijini leo.
Wananchi wakijichagulia bidhaa za kununua ndani ya tsn Super market Tegeta, mara baada ya kuzinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, Tegeta jijini leo.
Mwenyekiti wa Makampuni ya tsn, Forough Baghozah (kushoto), akifuria jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC, Boni Nyoni, wakati wakiondoka baada ya kumalizika hafla ya uzinduzi wa tsn Super market Tegeta jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
No comments:
Post a Comment