Katika mashindano ya mchezo wa Tennis ya Ufaransa, Roger Federer amefuzu kushiriki robo fainali kwa ushindi wa 5-7, 7-5, 6-2, 6-4 dhidi ya David Goffin wa Ubelgiji.
Mchezaji huyo anayeshikilia namba ya tatu kwa ubora Duniani sasa atapambana na mshindi wa pambano la Juan Martin del Potro wa Argentina na Tomas Berdych wa Jamhuri ya Czech kuania nafasi ya kushiriki nusu fainali.
Wakati huo huo mchezaji namba moja Duniani, Novak Djokovic amependezesha mchuano wa kufuzu kuingia robo fainali licha ya mpinzani wake Andreas Seppi kuongoza seti mbili za mwanzo 4-6, 6-7 lakini aliweza kutumia umahiri wake na kushinda seti za mwisho 6-3, 7-5, 6-3.
Mchezaji huyo bora hata hivyo alionekana mchovu asiyekua katika hali ya ushindani akitishia kua anayeweza kuanguka kwenye hatua hii.
Djokovic, anayetazamia kukamilisha idadi ya Vikombe vya mashindano ya kiwango cha 'grand slam' kwa kushinda Ufaransa, atachuana na mshindi kati ya Stanislas Wawrinka na Jo-Wilfried Tsonga.
Katika mashindano ya wanawake mchezaji namba moja Victoria Azarenka alikiri kua kila alichojaribu kukifanya kilikwenda kombo uwanjani na hivyo kuondolewa kwenye mashindano ya mwaka huu ya Ufaransa na Dominika Cibulkova.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alifululiza ushindi mara 26 mwanzoni mwa mwaka 2012 ikiwa ni pamoja na kushinda ngao yake ya kwanza kwenye kinyanganyiro cha Australia.
Wiki hii nzima Azarenka ahakuonyesha kiwango cha mchezo aliouonyesha mapema mwaka huu ikiashiria angeweza hata kutupwa nje mapema.
No comments:
Post a Comment