TANGAZO


Saturday, June 16, 2012

Croatia yaadhibiwa na UEFA

Italia na Croatia
Italia na Croatia
Shirika linalotawala soka barani Ulaya,(Uefa) limeitoza faini ya Euro 25,000 chama cha mpira cha Croatia kwa ghasia zilizozushwa na mashabiki wake wakati wa pambano kati ya Timu yao na Jamhuri ya Ireland.
Mashabiki wa Croatia walirusha fashfash wakati wa mechi hio mjini Poznan iliyomalizika kwa ushindi wa 3-1 jumapili iliyopita.
Mashabiki wa Croatia
Mashabiki wa Croatia
Wahudumu wa uwanja walikabiliana na mashabiki waliovunja uzio na moja kwa moja kwenda kumbusu Kocha wa Timu ya Taifa Slaven Bilic.
"hukumu hii imechukuliwa kwa sababu mashabiki waliasha moto na kurusha fashifashi na mizinga pamoja na kuvamia uwanja,imesema taarifa ya Uefa.
Wakati huo huo Uefa inachunguza madai kwamba ndizi ilirushwa uwanjani wakati wa mechi ya kundi C kati ya Italia na Croatia siku ya Alhamisi.
Mpiga picha mmoja alishuhudia wahudumu wa uwanja wakiokota ndizi na kusikia miliyo ya nyani iliyoelekezwa mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli.
Croatia itapambana na bingwa wa Dunia na pia wa Ulaya Uhispania katika mechi ya mwisho ya makundi siku ya jumatatu mjini Gdansk.
Ushindi au sare ya 2-2 itaiwezesha Croatia kusonga mbele kujiunga na Timu nane zilizovuka hatua ya makundi.

No comments:

Post a Comment