Kundi la mwanzo la Wasudan Kusini waliosubiri kwa miezi kadha kwenye kambi ya Sudan, wameanza safari ya kurudi nyumbani.
Wakuu wa Sudan walisema mwezi uliopita, kwamba watu hao ni tishio kwa usalama wa nchi.
Walipewa muda wa kuondoka nchini lakini amri hiyo baadae ilibadilishwa.
Wasudan Kusini walipoteza haki yao ya uraia baada ya Sudan Kusini kujitenga na kaskazini mwaka jana.
No comments:
Post a Comment