Klabu ya Manchester City
imemwomba msamaha kocha wa klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson
baada ya mshambulizi wao Carlos Tevez kuonekana akiwa amebeba bango
lenye Maandishi Rest In Peace Fergie, au lala mahala pema peponi Fergie.
Tevez amkejeli Sir Ferguson
Tevez alibeba bango hilo kubwa wakati wa sherehe za klabu ya City baada ya kushinda taji la ligi kuu nchini England.
Lakini kitendo hicho cha Tevez kinasaidikwa kuwa ni jibu kwa usema wa Ferguson aliotoa mwaka 2009 pale alipoulizwa kama kuna siku Manchester City itakuwa mbele ya timu yake Manchester United. Wakati huo mkufunzi Ferguson alijibu kwamba hilo haliwezi kufanyika wakati wa uhai wake.
Hata hivyo Tevez mwenyewe alisema baadaye kwamba haku-kusudia kumkosea heshima Sir Alex ferguson.
No comments:
Post a Comment