CHAMA
cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinaungana na
familia na wanahabari wote nchini kuomboleza kifo cha Mhariri wa Habari
za Michezo wa gazeti la Mtanzania Rachel Mwiligwa.
TASWA
imeshtushwa taarifa za kifo cha Rachel kilichotokea usiku wa kuamkia
leo, hivyo tunatoa pole kwa familia yake, waandishi wa habari za michezo
na wafanyakazi wenzake wote, wasanii na wanamichezo wengine katika
kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mdau mkubwa wa michezo na
burudani.
Kutokana
na msiba huo, chama kinaandaa taratibu zake za kuwasilisha rambirambi
kwa namna tulivyojiwekea, kwani marehemu hadi mauti yanamkuta alikuwa
mwanachama mtiifu wa TASWA. Hivyo upo utaratibu kama mwenzetu
akitangulia mbele ya haki namna gani tunatakiwa tufanye.
Lakini
pia upo utaratibu mwingine nje ya chama ambao utahusu mtu binafsi
kuwasilisha michango ya rambirambi, ambapo TASWA inawasiliana na
wahariri wote wa habari za michezo wasaidie kukusanya michango ya
rambirambi kwenye vyombo vyao, ambayo wataiwasilisha kwa wajumbe wa
Kamati Maalum ya kusimamia jambo hili.
Wajumbe
hao ni Angela Msangi ambaye atakuwa Mratibu akisaidiwa na Mwani
Nyangasa, ambao watashirikiana na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya
TASWA, George John ambaye ni Katibu Msaidizi wa TASWA, Grace Hoka na
Alfred Lucas ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Utendaji. Tunaomba
ushirikiano wa wadau katika kufanikisha jambo hili.
Msiba kwa sasa kwa mujibu wa taarifa za awali upo Manzese Tiptop,tutaendelea kujulishana kadri zitakavyopatikana taarifa mpya.
Tunaomba
waandishi wa habari za michezo, wasanii na wanamichezo kwa ujumla
tumuenzi Rachel kwa masuala mbalimbali aliyokuwa akiyatilia mkazo
ikiwemo kusimamia ukweli kwa kile alichokiamini na ndio maana tunasema
tutaendelea kumkumbuka daima. Mungu amuweke mahali pema peponi. Amin
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
No comments:
Post a Comment