Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Canada, Berly Oda, walipokutana kwa mazungumzo katika hoteli ya Sheraton jijini Addis Ababa ambako wote walihudhuria Kongamano la Kimataifa la Uchumi kwa Afrika. (Picha zote na Ikulu)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan baada ya kuhudhuria dhifa ya kitaifa waliyoandaliwa na mwenyeji wao, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi, jijini Addis Ababa Alhamisi usiku. Kulia kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Fedha wa Nigeria, Ngozi Okonjo-Iweala, wakati wa kielele cha Kongamano la Kimataifa la Uchumi kwa Afrika jana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bishara la Kimataifa - World Trade Organisation (WTO), Paschal Lamy walipokutana kwa mazungumzo katika hoteli ya Sheraton jijini Addis Ababa, ambako wote walihudhuria Kongamano la Kimataifa la Uchumi kwa Afrika.
No comments:
Post a Comment