Shirika la kujihami la NATO
limepinga ripoti inayolitaka kuchunguza vifo vya raia wa Libya waliouawa
katika harakati za jeshi la NATO mwaka jana. Shirika la kutetea haki za
binadamu Human Rights Watch limesema raia 72 waliuawa na kutaka NATO
kuwajibikia mauaji hayo.
Hata hivyo msemaji wa NATO amesema harakati za jeshi hilo ziliendeshwa kwa uwangalifu mkubwa hususan usalama wa raia.Katukio moja shambulio la bomu liliwaua watu 14 na baadaye watu wengine 18 waliokwenda kuwakoa majeruhi wakaangukiwa na bomu lingine na kufariki papo hapo.
NATO imesema iko tayari kushirikiana na utawala mpya wa Libya katika uchunguzi wa matukio ya mwaka jana.
Hata hivyo shirika hilo limepinga kuwajibikia mauaji hayo kwa sababu hakuna thibitisho kamili dhidi ya mauaji hayo.
No comments:
Post a Comment