Wajumbe wawili wa Jumuia ya Afrika Magharibi, ECOWAS, wameondoka Mali baada ya kushindwa kupata makubaliano, kuhusu nani anafaa kuongoza serikali ya mpito.
Rais wa muda, Dioncounda Traore, aliteuliwa mwezi uliopita baada ya kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi kuridhi kuondoka.
ECOWAS inasema Bwana Traore anafaa kuruhusiwa kuendelea na urais, baada ya muda wa awali, wa siku 40 kumalizika.
Viongozi wa mapinduzi, ambao bado wana madaraka, hawataki.
Mali hivi sasa imegawika pande mbili - eneo la kaskazini linadhibitiwa na wapiganaji wa kabila la Tuareg.
No comments:
Post a Comment